FANYA UNACHOPENDA


 

Mara nyingi watu hupenda kufanya kazi fulani kwa sababu aidha ya kifedha au kutafuta umaarufu au pengine kwa kulazimishwa na wazazi.

Lakini kazi hizi huwa hawazifanyi kutoka moyoni au Wala huwa haziwapi motisha. Ni muhimu sana ufanye kitu unachopenda kuliko kulazimisha au kulazimishwa kufanya kitu usichopenda.

Kama ni fedha au umaarufu utaupata kwa kufanya usichopenda, ila ndani mwako utakuwa unahisi kama kuna kitu hakiko sawa mara zote. Na kitu hiki kikiendelea kwa muda mrefu utajikuta ukiishi kama vile huishi. Yaani, utakuwa mtupu.

Ndiyo maana Benjamin Franklin aliwahi kusema kwamba kuna watu wanakufa wakiwa na miaka 25 na kuzikwa wakiwa na miaka 75. Mojawapo ya kitu kinachowafanya watu wafe wakiwa na miaka 25 ni kwa sababu wanafanya kitu wasichopenda. Hivyo, wanapita tu kwenye maisha wakiwa wanafanya kazi au kitu ambacho hakiwapi ukamilifu wa ndani.

Kazi ya kufanya leo. Tafuta kitu au kazi unayopenda na Anza kufanya hiyo. Inaweza ikawa haikulipi vizuri leo ila baada ya muda itaweza kukulipa vizuri kwa sababu utakuwa unaifanya kutoka moyoni tena kwa nguvu na akili zote.

Kazi usiyoipenda utaifanya sawa, lakini inaweza kwa kuwa haitoki moyoni, ufanisi kwenye hiyo kazi utakuwa ukipunguka kidogo kidogo bila ya wewe kujua. Mwisho wa siku utajikuta  umeingia pabaya.

GODIUS RWEYONGEZA

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X