Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia


Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao. 

Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao  unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni nguvu ya kuonana.

Hapa sizungumzii kuonana kwa Skype Wala zoom, bali kuonana ana kwa ana.

Ndiyo. Bado kuonana ana kwa ana kuna nguvu kwelikweli.  Katika zama hizi, kama una jambo lako la nguvu unataka kuongea na mtu, ni muhimu uonane naye ana kwa ana.

Ni rahisi kufikia uamuzi bora unapokuwa na mtu ana kwa ana kuliko anavyokuwa mbali.

Kanuni muhimu ambayo binafsi huwa inaniongoza ni hii hapa.
Kama unaweza kuonana na mtu ana kwa ana, usipige simu.
Kama unaweza kupiga simu, usitume ujumbe.

Kumbe ujumbe mfupi wa sms au whatsap uwe ni njia ya mwisho unayoweza kutumia baada ya kuona njia nyingine zimeshindikana.

Karibu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X