Vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya


Katika maisha Kuna vitu hata iweje huwezi kusema umechoka kuvifanya. Huwezi kusema nimechoka kupumua, maana ykiacha kupumua tu huo ndio mwisho wako. Huwezi kusema nimechoka kula, wala huwezi kusema nimechoka kulala, kuanzia leo sitalala tena. Ni vitu vya asili ambavyo mwili wako unahitaji ili uendelee kuwa imara zaidi.

Wewe pia Kuna vitu unapaswa kujiwekea utaratibu wa kuvifanya bila kuchoka. Ifuatayo ni orodha ya vitu ambavyo hupaswi kuchoka kufanya.

1. Usichokwe kuweka akiba wala kuwekeza.

2. Usichoke kusoma vitabu maana vutakusaidia kuongeza maarifa, ufahamu na kipato.

3. Usichoke kusamehe maana kutosamehe kunakuumiza wewe mwenyewe.

4. Usichoke kuongeza kipato chako.

5. Usichoke kutengeneza bidhaa bora zaidi

6. Usichoke kutoa huduma nzuri

7. Usichoke kushukuru

8. Usichoke kusema ukweli

9. Usichoke kuisimamia ndoto yako.

Rafiki yangu, hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo hupaswi kuchoka kuvifanya. Unaweza kuongeza vingine zaidi.

Je, umeshapata vitabu vipi vya kwangu vya kiswahili.

Chagua vitano Leo kwa elfu kumi tu.

Ingia hapa uchague 

https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393

kisha ulipie elfu kumi kupata vitabu hivyo vitano.

Lipia kwa Airtel money 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X