Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine.
Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu.
1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako.
2. Fahamu kuwa maisha ni wajibu wako Wala siyo mzazi, mme, mke, shangazi n.k.
Ukishindwa ni juu yako na ukishinda ni juu yako pia. Pambana mara zote kufanikiwa kifedha.
3. Kwa kila kiasi cha fedha unachopokea bila kujali ni kidogo kiasi gani, hakikisha unaweka akiba. Akiba haiozi.
4. Tengeneza vyanzo mbalimbali vya kipato vitakavyokusaidia kuongeza kipato chako. Kuwa navyo hata kama Ni vidogo, vutakusaidia.
5. Fedha inafuata sana kanuni ya aliyenacho anaongezewa zaidi. Ukiwa na fedha ni rahisi kupata fedha, kuliko pale unapokuwa huna fedha. Hivyo pambana mara zote kuwa nazo.
Soma zaidi: TUKUZE AKAUNTI ZETU AISEE