Rafiki yangu, najua unafahamu kuwa una uhuru wa kuchagua chochote kile unachotaka kuwa. Unaweza kuchagua kuwa mwalimu, mchekeshaji, mshereheshaji, dereva, mkulima, mwanamichezo, mwanasiasa, mwanaharakati au chochote kile. Huo uhuru unao na wala hakuna mwenye uwezo wa kukuzuia wewe kwenye hilo.
Hata hivyo, kuna kitu kimoja tu ambacho ningependa kukutahadharisha, na kitu hiki siyo kingine bali kuchagua kuwa mlaji tu. Haupaswi kuwa mlaji wa kazi za watu wengine tu, hila wewe kuzalisha kazi.
Kwa kitu chochote kile ambacho umechagua kwenye maisha, hakikisha unachagua kuwa mzalishaji.
Dunia tunayoishi, haipungukiwi hata kidogo na walaji, ila wazalishaji ndio wachache. Wewe kuwa huu upande wa wazalishaji
Kama ulizoea kuingia YouTube na kuangalia video tu, kisha kuondoka, sasa ni zamu yako pia ya kuzalisha.
Kama ulizoea kusoma vitabu vya watu wengine, na wewe zalisha hata kwa kutupa mrejesho juu ya mambo uliyojifunza kwenye vitabu husika.
Rafiki yangu, kuanzia leo. Anza kuwa mzalishaji.
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri