Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa


Leo napenda kumtambulisha kwako mwajiriwa mtiifu kuliko wote duniani,  anafanya kazi kwa saa 24 siku saba za wiki. Hadai mshahara wala marupurupu yoyote. Yeye anachojua ni kufanya kazi kwa bidii kila wakati na kutoa matokeo kadiri unavyomwelekeza. Nimekuwa namtumia mwajiriwa huyu kwa siku nyingi sasa na hizi ndizo sifa nilizobaini kwake.

Anaweza kusalimia wateja,
Anaweza kueleza jinsi bidhaa zangu zinavyofanya kazi
Anajibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Anatoa mawasiliano yangu ya wateja wanaohitaji kufahamu zaidi kuhusu huduma zangu.
Anatoa shuhuda za watu walionufaika na kazi zangu.
Anatoa maelekezo ya jinsi ya kulipia huduma zangu au vitabu vyangu.

Kama kuna kitu kingine cha ziada, bado anaweza kukifanya. Mwajiriwa huyu siyo mwingine bali ni tovuti na blogu.
Kimojawapo kati ya hivi kinaweza kukupa matokeo ila kwa upande wangu natumia blogu.

Soma zaidi tofauti Kati ya tovuti na blogu.

Nikiandika kitu kwenye blogu yangu leo hii, hakibadiliki wala kutoweka labda pale nitakapoamua kufanya hivyo. Kama ni ujumbe wa kuelimisha kama huu utaendelea kuwa hewani. Utasomwa leo hii na utasomwa miaka mitano ijayo bila kubadilika.

Hii ndio maana na wewe unahitaji kuwa blogu. Ebu kwa mfano jiulize status yako ya whatsap uliyoandika januari mosi, 2022 iko wapi? Kwa mfano kama kuna mtu aliisoma na akaipenda na leo hii angependa kurejea tena kuiona atafanyaje kuiona? Kiufupi, jibu ni haiwezekani.

Sasa mambo ni tofauti kwa blogu. Yenyewe ukiweka kitu hakitoweki baada ya saa 24 au baada ya muda fulani. Kinaendelea kuwepo. Kama mtu atakisoma au kukisikiliza leo, anaweza pia kurejea kwake miaka kadhaa mbeleni na kusoma tena.

Blogu inafanya kazi saa 24 kwa siku Saba 7 za wiki.

Mtu akiingia mtandaoni usiku na kufungua blogu yako, atanufaika sawasawa na yule atayeingia wakati wa jua kali saa saba mchana.

Blogu yenyewe inafanya kazi bila kujali kuna baridi au mvua.

Kwenye blogu unaweza kuweka makala au mafunzo kuhusu bidhaa au huduma zako.
Unaweza kuwapa watu maelekezo ya namna ya kununua bidhaa yako yoyote.
Unaweza kuwaelekeza watu jinsi ya kuwasiliana na wewe au watu wengine.
Unaweza kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara n.k.

Kwa hakika blogu ni mwajiriwa mzuri ambaye unaweza kumtumia kwenye biashara yako na akafanya kazi bila kuchoka.
Je, wewe upo tayari kumtumia mwajiriwa huyu?

Karibu nikutengenezee blogu yako leo hii. Tuwasiliane kwa 0755848391 

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


2 responses to “Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X