Juzi tarehe 19 ilikuwa ni siku rasmi ambapo watu wengi huwa wanaacha kufanyia kazi malengo yao na kuanza kuishi maisha ya kawaida. Hii siyo siku ambayo nimeibuni bali ni kutokana na tafiti kuntu zilizofanywa na watafiti wanaoaminika duniani. Na siyo kwamba zimefanywa kwa watu kumi au ishirini, bali zimefanyika kwa watu zaidi ya milioni 800. Ndio milioni mia nane!
Katika kuwafuatilia watu hawa, iligundukilika kuwa WATU HAWA WANAKUWA NA MOTISHA KUBWA sana wanapoanza mwaka mpya, ila motisha hiyo inapungua zaidi na kwa wengi siku ya 19 ndipo wanaagana kabisa na malengo yao.
Sasa kwa nini watu huwa wanaachana na malengo yao mapema? Hiki ndicho naenda kueleza kwenye makala ya leo.
Kwanza ni kuwa na matamanio makubwa huku wakipenda kupata matokeo ya haraka. Mtu anaanza mwaka mpya akiwa na unene wa kupitiliza, anapoanza mwaka anaweka malengo ya kuagana na unene wake huku akiwa anataka kuagana na unene huo ndani ya siku chache tu. Baada ya hapo anaanza mazoezi, ila ndani ya siku 14 za kwanza kunakuwa hakuna mabadiliko yotote ya maana anayoyaona, anaanza kuvunjika moyo. Mpaka siku ya 18 bado pia kunakuwa hakuna kitu kikubwa akbacho kimeonekana. Mtu anaamua kuagana na malengo yake na hiyo inakuwa imeishia hapo.
Ambacho huyu mtu anasahau ni kwamba kufanyia kazi na kufikia malengo kunahitaji mchakato. Mwanzoni kabisa unaweza usione matokeo yotote, Ni mpaka pale utakapong’ang’ania tena na tena, ndipo matokeo yataanza kujitokeza.
Siku 18 za kwanza zinakuwa bado sana kwa wewe kuachana na malengo yako.
Pili, ni msukumo wa vyombo vya habari.
Mwishoni mwa mwaka vyombo vya habari vinasisitiza sana kuhusu malengo na neno MWAKA MPYA linaibwa sana. Watu mpaka wanafundishwa namna ya kuweka malengo, ila sasa ule mchakato wa kufanyia kazi malengo huwa unasahaulika. Na vyombo vyenyewe huwa haviendelei kuweka msisitizo baada ya mwaka mpya kufika. Na hicho ndicho huwa kinawafanya watu kuachana na malengo yao mapema.
Ninachotaka ufahamu ni kuwa malengo unayoweka yanapaswa kutoka ndani yako, wala kusiwepo na msukumo wa nje au mtu mwingine. Ukiwa na msukumo kutoka nje utaishia njiani mapema sana.
Hivyo ni vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kufanyia kazi malengo yao na kuachana nayo mapema. Viepuke ili uweze kufanyia kazi malengo yako mwaka huu na kuyakamilisha kwa kishindo.
SOMA ZAIDI: KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.🤷🏽♂🤷🏽♂
Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
One response to “Kwa Nini watu wengi husahau malengo ya mwaka mpya Mapema Sana”
[…] Kwa Nini watu wengi husahau malengo ya mwaka mpya Mapema Sana […]