Kauli ya mwak mpya na mambo mapya si kauli ngeni masikioni mwa watu. kila mwaka mpya unapoanza huwa unasikia watu wakiisema kauli hii tena kwa kujidai. Binafsi naiipenda pia kuauli hii, japo kuna watu ambao wanaitafsiri vibaya na hivyo kuitumia ndivyo sivyo.
Unakuta mtu kila mwaka mpya unapoanza yeye anakazana kuhakikisha kwamba anaanza kitu kipya kwa kusema kwamba ni mwaka mpya na kuachana na vitu ambavyo alikuwa akifanya hapo mwanzo. Kama ni fursa utakuta mtu anakimbizana kudaka fursa mpya na kuachana na ile ya zamani.
Ubaya wa hiki kitu ni kwamba kinakufanya ushindwe kubobea na watu wanashindw akukuelewa kuwa wewe ni mtu wa aina gani.
Tafsri nzuri ya mwka mpya na mambo mapya ni kwamba unapaswa kuongeza juhudi zaidi kwenye kile ambacho wewe umekuwa unafanya kwa siku zote. Nyingine ni kwamba unapaswa kufanya mambo mapya kwa kuachana na tabia mbovu ambazo zilikuwa zinakuzuia wewe kusonga mbele na kufikia mafanikio makubwa, badala yake unapaswa kuendelea kushikiliai tabia ambzo zitakufanya uzidi kusonga mbele zaidi.
Tafsiri nzuri ya mwaka mpya na mambo mapya ni kwamba unapaswa kutoa huduma kwa viwango vya hali ya juu sana (viwango vya nyota tano).
Tafsiri ya mwaka mpya na mambo mapya ni kwamba kama kuna kitu kitu ulikuwa unakifanya kwa namna ya ukawaida sana, sasa unapaswa kuanza kukifanya kwa viwango vikubwa tena vya hali ya juu sana.
Kama ulikuwa na tabia mbaya (kaa kuvuta bangi na kunywa pombe) achana nazo.
Hiyo ndiyo tafsiri nzuri y mwaka mpya na mambo mapya, ila siyo kwamba kila mwaka wewe uwe unakimbizana na fursa mpya.
Nakutakia kila la kheri rafiki yangu. umekuwa nami rafiki yako wa ukweli, Godius Rweyongeza.