Sababu 03 Kwa Nini Mwezi Januari Unakuwa Mgumu Kwako


Januari ni mwezi wa kwanza wa kila mwaka. Mwezi unaofuata mara tu baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Mwezi wenyewe wa januari unaanza kwa shamrashamra za kuushangilia mwaka.

Ni mwezi ambapo watu wanakuwa wamejichana na kula bata siku chache kabla, huku wakiwa wametumia hata fedha ambazo hawakupaswa kutumia, kitu kinachowafanya waanze mwaka wakiwa wamefuria.

Watu wanaanza mwaka wakiwa hawana fedha huku upande mwingine fedha zikiwa zinahitajika sana.
Kuanzia ada za watoto, kodi za nyumba, na mambo mengine

Vyote hivyo vinahitaji hela na wakati huohuo   mahitaji mengine ya kawaida kama chakula, umeme, kulala, vikiwa vinahitaji hela pia. Hicho kitu kinawafanya watu wachanganyikiwe.

Kuna utani mtandaoni unaosema

Watu wafupi mwezi huu mnatupa shida, ukiwa barabarani unatembea unamwona mtu mfupi, unadhani mwanao karudishwa nyumbani kwa sababu ya ada.

Utani mwingine unasema,
Kuna ile minyoo ambayo ukiwa nayo unakosa hamu ya kula. Naipataje, maana hii ni januari?

Wakati hizo kauli hizi mbili zimekaa kiutani, utani tu, ila pia zimebeba ujumbe mzito kuhusu uhalisia wa watu wengi walivyo mfukoni.

Kwenye makala hii ninaenda kukuonesha kwa nini umefulia mwezi huu wa Januari na hatua za kuchukua ili kuondokana na hiyo hali.

1. Umefulia kwa sababu unategemea chanzo kimoja cha kipato.
Hakikisha unakuwa na vyanzo vya kipato zaidi ya kimoja, vitakusaidia kuondokana na ukata.

2. Umefulia kwa sababu ulitumia fedha nyingi mwishoni mwa mwaka.ulitumia hata fedha ambazo hakupaswa kutumia.

Suluhisho: kuanzia januari hii anza kuweka akiba maalumu utakayotumia mwishoni mwa mwaka.  Na akiba nyingine kama ambavyo nimekuwa nikikushauri. Na uwe na na nidhamu ya fedha, usitumie fedha za malengo yako mengine kwa ajili kula bata

3. Umefulia kwa sababu huna hela za kulipa ada za watoto.

Suluhisho: naomba ufahamu kuwa suala zima la ada za watoto, halipaswi kuwa kitu kigeni kwako. Ni kitu ambacho unakuwa unakifahamu kuanzia januari mpaka disemba. Hivyo kwa mwaka huu uanze kujiandaa kwa kuweka pembeni fedha kidogo kidogo maalumu tu kwa ajili ya ada za watoto.

Hizo Ni baadhi ya sababu ambazo zinakufanya ufurie januari hii, ziepuke kwa manufaa yako ya sasa na miaka ijayo. Kila la kheri.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X