USHAURI MUHIMU: Kama una ndoto ya kuwa mwandishi na unawaza nani ATAHARIRI, ATACHAPA na jinsi utakavyouza kazi zako Basi Soma hapa.


Siku ya leo najibu swali nililoulizwa na mmoja wa wasomaji wangu. Anasema;

Hi Godius.
Naitwa Juma Mazengo Malale, kwa sasa nipo Shinyanga, ndoto yangu nikuwa mwandishi wa vitabu. Mpaka sasa nipo kwenye mchakato, changamoto ipo kwenye mambo kama haya.
1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?

 

Habari yangu ni njema ndugu yangu. Karibu kwenye ulimwengu wa waandishi na hongera sana kwa hatua hiyo uliyoamua ya kuwa mwandishi.

Hata hivyo pongezi zangu hupaswi kuzichukua zote kwa sababu kwa maelezo yako, inaonekana umeamua kuanza kuandika ila bado hujaanza kuandika; kitu ambacho ni muhimu sana,  linapokuja suala zima la uandishi.

Kiufupi hakuna mtu anaitwa mwandishi kwa sababu eti anatamani kuwa mwandishi au kwa sababu ana mpango wa kuja kuwa mwandishi siku moja. Kama ilivyo kweli kwamba hakuna mtu anaitwa mwanasheria kwa kutamani kuwa mwanasheria bali kwa sababu ameingia darasani, amesomea, amefuzu na anafanyia kazi fani yake.

Mwandishi ni mwandishi kwa sababu anaandika. Kwa hiyo, nataka na wewe uanze kuitwa mwandishi tena kuanzia leo, na utaweza hilo kwa kuanza kuandika.

Hatua hiyo moja tu itaweza kukufungulia fursa za kujua vitu vingine vingi. Kwenye swali lako umeuliza

1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?

Naweza kuanza kujibu maswali hayo baada ya kujihakikishia kuwa umeanza kuandika.

Kwa kuwa najua baada ya kusoma hapa utaendelea mbele na kuanza kuandika , basi acha niendelee kukujuza zaidi, ila sharti langu kwako ni moja tu. Uweke mpango wa kuandika mara tu baada ya kusoma makala haya.

UTAANDIKA KUHUSU NINI
Kuna maeneo mengi ambayo wewe unaweza kuandikia. Unaweza kuandika mengi kuhusu
πŸ‘‰maisha yako (maisha yako ni ya tofauti sana, unaweza kuwa unayachukulia poa, ila kuna mengi kutokana na maisha yako ambayo yanaweza kuwa msaada kwa watu wengine).

πŸ‘‰ Unaweza kuandika kuhusu ujuzi ulio nao ambao uliwahi kuupata kwa kufanya kazi fulani.

πŸ‘‰ Unaweza kuandikia eneo la taaluma yako. Kama kuna vitu umejifunza basi kuna watu wengine ambao wangependa kuvifahamu kwa kina hivyo vitu, unaweza kuwaelimisha watu kuhusu hivyo vitu kupitia maandishi yako.

πŸ‘‰ Unaweza kuandika kuhusu kitu unachopenda kufuatilia. Kama kuna kitu unapenda kufuatilia, basi unaweza kuamua kuzama ndani zaidi ili kukifuatilia hicho kitu huku ukiwa unawajuza wengine kwa kuwaandikia.

πŸ‘‰ Yapo mambo mengine ya kuandikia, ila kwa leo hayo yatoshe. Mengine utayasoma kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.

NANI ATAHARIRI KAZI YANGU
Wewe ndiye unapaswa kuwa mhariri wa kazi yako ukiwa mtu wa kwanza. Pia kuna wahariri watalaam ambao utawasiliana nao baada ya kukamilisha kazi yako, nao watakuwa tayari kukusaidia. Hivyo, Anza kuandika kwanza, ukifikia hatua ya uhariri wa kazi yako, itakuwa rahisi tu kukuunganisha na wahariri

NANI ATACHAPA KAZI YAKO
Wachapaji pia wapo wa kutosha. Anza kuandika kwanza na soma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ili uweze  kupata zaidi mambo mengine kwa undani.

NITAMUDU GHARAMA
Ndio utaweza kumudu gharama.

KITABU KIBEBE PAGE NGAPI.
Itategemea unandikia nini na unataka kueleza mada kiundani kiasi gani. Binafsi nikiwa naandika kitabu huwa sifikirii sana kuhusu kurasa za kitabu. Ila huwa nafikiria zaidi kuhusu kile nilichonacho kuhusu mada husika. Huwa najitahidi kuandika kila kitu ninachojua na mwisho wa siku upande wa kurasa huwa unajipanga wenyewe. Ila kwa kuwa umeuliza kuhusu kurasa, basi acha nikwambie kwamba viwango vya kimataifa vya kuita kitu kitabu ni kurasa 50. Ila hili lisikuwazishe sana, Anza kuandika kwanza mambo mengine yanajipanga kadiri utakavyoendelea.

Kwa leo inatosha na ninakomea hapo. Hata hivyo, nakushauri sana, usome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Kitabu hiki kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na makala.

Kipate kitabu hiki kwa 6,500/- tu. Kupata kitabu hiki utatuma hicho kiasi kupitia 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Morogoro-Tz

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X