USIPOJITAMBUA, KUNA WATU WACHACHE WANAOJITAMBUA WATAKUTUMIA WANAVYOTAKA


Kuna stori moja ya mchungaji huko Nigeria, ambayo nimelazimika nikushikirishe kwa lengo la kukwambia kitu. Na stori hii ni ya mchungaji Dr. JS Yusuf wa Nigeria ambaye yeye ameanzisha utaratibu wa kuuza chupi kwa wanawake. Chupi hizi zina picha yake na anasema kwamba, mwanamke yeyote atakayevaa chupi hizi, atakuwa na mvuto kwa wanaume na ataweza kumpata mwanaume bora, asiyedanganya, na Wala hawezi kuachika. 

Kiufupi, mchungaji anawahidi wanawake kuwa wakivaa chupi zake, basi hawatakuwa na maumivu yoyote ya moyo na pia itawakinga dhidi ya magonjwa. Na chupi hizi zinauziwa madhabahuni.

Kutokana na kijistori hiki, nimeona niseme haya ili yaweze kukusaidia.

Kwenye dunia hii kujitambua ni muhimu sana, unapaswa kufanya chini juu, kuhakikisha kwamba unakuwa na ndoto kubwa na kusudi la kuwa hapa duniani na kujiweka bize na mambo yako. 

USIPOJITAMBUA kuna watu wachache wanaojitambua watakutumia wewe, kadiri watakavyo. Watakuendesha na wewe utaendesheka. Mfano mzuri unaweza kuuona kwa wanasiasa. Huwa wanawaendesha wafuasi wao kwa sera na maoni ya hapa na pale. Leo anaweza kusema hili, wafuasi wake wakashangilia, na kesho yake akasema lile wafuasi wakashangilia. 

Pia, ujifunze kuwa na msimamo na kusimamia ndoto zetu, malengo na kusudi la maisha yetu. Usiwe mtu wa kuyumbishwa, usiwe bendera hufuata upepo.

Tatu, fahamu kuwa nguvu ya kweli ya kukusaidia wewe kusonga mbele, tayari unayo. Ndio maana James Allen aliwahi kusema; ugunduzi mkubwa niliougundua kwenye zama zangu ni kuwa binadamu ana uwezo mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri. Na watalaamu wengi wamethibitisha hili. Utafiti mwingine umeonesha kuwa watu wengi wanatumia chini ya asilimia kumi ya uwezo wao. Hata wale unaowaona  kama wamefanya makubwa, jua kabisa wametumia chini ya asilimia kumi.

Kwa hiyo, wewe tayari unao uwezo mkubwa ndani yako. Ila sasa ukikaa na kuanza kusubiri sijui chupi ziamshe uwezo huo, utasubiri sana. Nashauri uwe mtu wa kutumia nguvu na uwezo ulionao. Anza leo.

Nashauri uanze kusoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Pata hardcopy kwa elfu 20 tu. Na soft copy kwa elfu kumi.

SOMA ZAIDI:  Jinsi ya kuwa na fedha kama serikali

Jitambue uoke maisha yako. Wasiliana nami leo kupata nakala yako kupitia 0755848391.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X