Mwaka 1937 ni mwaka muhimu sana kwenye ulimwengu wa mafanikio. Ni mwaka ambao kitabu cha THINK AND GROW RICH kilichapwa baada ya miaka mingi ya utafiti.
Kwenye kitabu hiki mwandishi ameeleza mbinu za mafanikio ambazo ziliwapa utajiri mkubwa sana matajiri wa wakati huo. Hapa wanaongelewa watu kama kama akina Rockefeller ambaye mpaka leo hii amebaki kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa kuwahi kutokea.
Kutokea hapo kitabu hicho kimetengeneza matajiri wengi sana, na kimewasaidia wengi kufika mbali.
Kitabu kimeeleza hatua 13 za kufikia mafanikio makubwa. Mwandishi anasema unapaswa kuwa na
1. Shauku ya kufanikiwa
2. Unapaswa kuwa na imani
3. Unapaswa kujinenea maneno chanya
4. Unapaswa kuwa na elimu/maarifa sahihi
5. Unapaswa kuwa mvumilivu
6. Unapaswa kuungana na timu ya watu sahihi na mengineyo.
Ila sasa kuwa na hayo yote haitoshi. Hapo ndipo mwandishi anakwambia kwamba; chanzo cha mafanikio yoyote kipo kwenye WAZO. Ukishakuwa na wazo ndipo sasa utaliunganisha na shauku yako ya kufanikiwa. Ndipo utapaswa kuwa na imani kuwa utakifanikisha.
Hapo ndipo utapaswa pia kujinenea maneno chanya na mengineyo.
Kwa hiyo, kama unataka kufanikiwa Anza kwa kujiuliza hivi mimi nina wazo gani haswa la kunisaidia kufanikiwa? Kama huna wazo jifikirie tena.
Wazo lako ndio chanzo kikuu cha kupata mafanikio unayotaka.
PATA KITABU CHA BURE
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
+255755848391/ Morogoro-Tanzania