Karibu kwenye Duka La Mtandaoni La Songa Mbele


Kuna msemo mmoja wa kilatini unasema kwamba furahi na wanaofurahi, huzunika na wanaohuzunika.

Sasa leo hii siyo kwamba nahuzunika bali nina furaha na mimi nimeona nikukaribishe wewe ili nikumegee hii furaha. Si unajua hivi vitu vinaambukizwa?

Furaha yangu ni kutangaza duka la mtandaoni ambapo wewe au mtu yeyote anaweza kuingia na kununua bidhaa itakayokuwa inapatikana humo.

Kwenye duka hili la mtandaoni kutakuwa na bidhaa za aina tatu tu.

Mafunzo kwa njia ya makala au ebooks
Mafunzo kwa njia ya sauti (audio) na
Mafunzo kwa njia ya video.

Kama ni makala basi itakuwa inajadili mada moja kwa undani kabisa ili wewe uweze kuielewa.
Kama ni audio basi itakuwa pia imezama ndani kujadili kitu fulani na itakuwa siyo chini ya dakika 30.
Kama ni video bsi na yenyewe haitakuwa chini ya dakika 20.

Na itakuwa ni kila wiki unapata kitu kimojawapo kati ya hivyo kwenye hili duka.

Vigezo na masharti

Huwa ukiingia kunua vidhaa kwenye tovuti yoyote ile ni lazima huwa unakuta kuna vigezo na masharti vingi kweli.
Aidha kwa upande wangu kwa sasa nimeamua kuwa kigezo na masharti kitakuwa kimoja tu. Kama vitahitajika vingine basi vitaongezwa baadaye ila kwa sasa, kigezo na masharti Ni kwamba ukinunua bidhaa yotote kwenye duka letu na ukapata bidhaa inayoenda kinyume na matarajio yako au bidhaa iliyo chini ya viwango  Basi nitakulipa mimi.
Yaani, utakurudishiwa fedha zako na nitakuongezea fedha nyingine kama hizo ulizolipia bidhaa hiyo. Hivyo, utapokea fedha yako na ya ziada. Kama ulitoa elfu tano basi utarudiahiwa elfu kumi, tena bila kuulizwa maswali.

Na simaanishi hili kwa udogo, nalimaanisha haswa. Hicho ndiyo kigezo ambacho naenda kujitoa kuhakikisha kinakamilika bila kujali napitia katika hali gani kwa wakati husika na sisemi hilo ili nikushawishi ukanunue bidhaa leo hii.

Ila nasema hivi, “hicho ndiyo kigezo na kiwango nilichojiwekea”, hivyo wewe ununue au usinunue, mimi nitaendelea kusimamia hicho kigezo kila siku ya maisha yangu.

Nimeamua nijitoe hivyo.

Kwa sasa hivi kuna bidhaa gani kwenye duka? Kwa sasa kuna ebook ya MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA tu. Nyingine zitaendelea kuwekwa kadiri muda unavyoenda.

Je, naweza kununua bidhaa moja kwa moja kwenye duka hili?
K
wa sasa bado halijakaa kwa mfumo unaokuwezesha wewe kununua bidhaa moja kwa moja. Hivyo, kwa Sasa ukihitaji bidhaa yoyote ile, tuwasiliane kwa simu 0755848391 ili nikutumie. Tutaendelea kuliboresha duka letu mpaka uweze kununua moja kwa moja bila kuhitaji msaada zaidi Kutoka kwangu.

Je, unapenda kupata ebook ya MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA? BONYEZA HAPA

Kupaya mafunzo Zaidi: BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X