Kitu Gani Haswa Kinahitajika Ili Kufanikisha Wazo Lako


Mwaka 1908 ni mwaka wa kihistoria maana ndio mwaka ambao gari la kwanza lilitengenezwa na kampuni ya Ford ambayo ilianzishwa mwaka 1903,

Gari hilo liliipa jina kampuni ya Ford na kuifanya itengeneze fedha za kutosha, kiasi kwamba watu wengi wakawa wanatamani kuanzisha biashara kampuni nyingine ambazo zingezalisha magari. Ukiangalia kwenye mtandao wa google, kampuni zilizoanzishwa kati ya mwaka 1900 mpaka 1999 ni karibia 3000.

Kiufupi biashara ya magari ilikuwa ni biashara nzuri, na wazo la kuanzisha biashara ya magari lilikuwa ni wazo zuri, ila cha kushangaza ni kwamba, biashara nyingi zilizoanzishwa miaka hiyo zilikufa. Tatizo lilikuwa ni nini wakati watu hawa walikuwa na wazo zuri la biashara?

Labda tatizo lilikuwa ni kwamba walichelewa kuwa na wazo hilo, labda Henry Ford alishateka soko na kuijua biashara kiundani hivyo walioingia kwenye biashara wakiwa wa ili hawakuweza kufanikisha hiyo biashara.

Hiki kitu kinanikumbusha mwaka 2005. Kampuni ya google ilikuwa tayari imeshajiorodhesha kwenye soko la hisa na ilikuwa na akiba ya fedha ya kutosha. Wafanyakazi wa kampuni wa kampuni hiyo walikuja na wazo la kutengeneza jukwaa ambalo watu wangekuwa wanashirikishana mawazo kwa njia ya video. Wazo hili lilikuwa ni kutengeneza kitu kama youtube ya leo. Na walianza kulifanyia kazi, wakiuita mtandao wao Google Video. Siku chache baadaye, vijana wawili walikuja kuanzisha mtandao wa youtube ambao ulikuja kuwa mkubwa na kuitupilia mbali Google video. Leo hii hata sijui kama wewe unaijua hiyo googlevideo, pengine ndio umeisikia leo kwa mara ya kwanza.

Sasa kitu gani kiliwafanya Google wafeli, wakati wenyewe ndio walikuwa watu wa kwanza kupata wazo hiilo kabla ya youtube? Kwa hiyo ni kitu gani sasa kinahitajika ili kuweza kufanikisha wazo lako? Mbona hata waliotangulia kuwa na wazo muda mwinginie nao wanafeli kwenye kile wanachofanya?

Labda tuseme kwamba kinachohitajika ili wazo lifanikiwe ni fedha za kutosha. Na hiki nacho ukikifuatilia kiudani utagundua kwamba siyo kweli, wakati kampuni ya google inaanzisha google video ilikuwa tayari na fedha nyingi kuliko hao vijana wawili waliokuja kuanzisha youtube baadaye, kwa hiyo suala zima la kusema kwamba wazo la biashara linafanikiwa kwa kuwa na fedha za kulifanyia kazi siyo kweli.

Nini sasa kinahitajika?

Kwanza, inahitajika utoe thamani. Watu hawatapenda kitu kwa sababu tu umesema kwamba hili ni wazo bora la biashara. Wazo lako bora la biashara watu hawana shida nalo. Ukiingia sokoni na kusema kwamba nina wazo bora la biashara hivyo naomba mnilipe, watu watakucheka tu na kuondoka.

Kitu kikubwa ambacho watu wanahitaji ni thamani inayotokana na hilo wazo. Kama biashara yako inatoa thamani basi watu watajipanga kuhakikisha kwamba wanapata hiyo thamani itokanayo na biashara yako.

Yaani, wazo lako la biashara linapaswa kuwa kama moto katikati ya baridi. Ukiwasha moto wakati watu wana baridi, ni lazima tu watajipanga kuja kuota huo moto. Sasa na biashara yako inapaswa kuwa hivyo, angalia ni thamani gani ya kipekee ambayo unaweza kutoa kwenye biashara yako na ikawa yenye manufaa kwa watu wengine.

Unahitaji kujiuliza hivi hili wazo langu la biashara nililonalo linatoa thamani gani kwa watu? Kama hakuna thamani inayotolewa na wazo lako hilo, unapaswa kukaa chini na kujiuliza tena kuhusu hilo wazo lako.

Pili, unahitaji ujitoe kabisa kwa ajili lya kulifanyia kazi wazo lako. Tena unapaswa, kujitoa pakubwa tu.

Tatu unapaswa kutafuta njia sahihi za kuwafikia watu sahihi wanaohitaji huduma inayotokana na wazo lako la biashara. Anza na watu wachache kwanza, kisha endelea kupanua.

Kwa leo naishia hapa, ila unachopaswa kufahamu ni kuwa unahitaji zaidi yay wazo la biashara, unahitaji zaidi ya fedha ili kufanikisha wazo lako na siyo lazima uwe mtu wa kwanza ili wazo lako hilo liweze kufanikiwa kwa viwango vikubwa.

PATA KITABU CHA BURE

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

+255755848391/ Morogoro-Tanzania


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X