Vitu Vinavyofanya Wengi Washindwe Kufikia Malengo Na Ndoto Zao


Kwanza ni kuiga watu wengine. Mwandishi wa vitabu John Mason, anasema kwamba imitation is limitatiom, akimaanisha kwamba kuiga ni kikwazo kikubwa sana ambacho kinawazuia watu wengi kuweza kufanyia kazi malengo na ndoto zao na hata kuweza kuzifikia. Ukweli ni kuwa, kama una malengo na ndoto kubwa, kamwe usiige wengine wanafanyaje. Badala yake amua kufanya vitu kwa staili yako mwenyewe.

Kuiga wengine ni kuamua kujiibia uwezomkubwa uliolala ndani yako.

Pili ni ni kukosa vipaumbele.

Unapokosa vipaumbele hata kama una majukumumengi unaweza  kujikukuta kwamba hufanyii chochote. Kwa nini?

Kwa sababu huna vipaumbele. Muda ambao unatakiwa kuwa unafanya kazi, unaingia instagram kuchati na huoni shida kwa sababu huna kipaumbele.

Muda ambao unapaswa kuwa unafanya kazi, anakuja mtu anakwambia kwamba mwende kuangalia mpira, kwa sababu huna vipaumbele, kwa muda huo kwako hicho ndiyo kinakuwa kipaumbele chako! Kwa hiyo mwisho wa siku unaweza kujikuta unaimaliza siku yako ukiwa umechoka. Lakini ni kitu gani cha maana ambacho umeweza kufanya ndani ya siku yako, kikiangaliwa kitu hicho, bado huwezi kukiona vizuri kwa sababu tu  HUNA VIPAUMBELE

Sikiliza maisha bila vipaumbele, siyo maisha ambayo unapasawa kuwa unaishi wewe.

Na vipaumbele vyako vinapaswa kuanzia kwenye ndoto zako. Unazijua ndoto zako?

Inashauriwa asilimia 80 ya muda wako uutumie kwenye kufanyia kazi malengo na ndoto zako.

Kama umeajiriwa zaidi ya asilimia 80 ya muda wako unapaswa kuitumia kwenye kufanya kazi za ofisi.

Kama umejiajiri zaidi ya asilimia 80 ya muda wako unapaswa kuutumia kwenye biashara yako.

Yaani,  kufanya kazi kunapaswa kuchukua sehemu kubwa ya muda wako kuliko kitu kingine chochote.

Kama kuna wakati utajikuta umekosa kipaumbele. Jiulize ni kitu gani nafanya sasa hivi kuelekea malengo yangu makubwa?

Kama hakuna kitu unafanya, basi huo utakuwa muda mzuri wa wewe kuhakikisha kwamba unafanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa zilizo mbele yako.

Imeandikwa na Godius Rweyongeza

Kupta vitabu vya Godius Rweyongeza wasiliana naye kwa 0684408755 sasa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X