Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

 • Kama una Simu Janja na huingizi Kipato, Unakosea hapa. Rekebisha Mara moja

  Siku Moja Robert Kiyosaki alisema kwamba kama una simu janja na Bado wewe ni maskini, basi fahamu wazi kuwa Kuna sehemu unakosea. Ukitafakari maneno ya Robert Kiyosaki unagudua Kuna ukweli mkubwa sana hasa katika ulimwengu wa Leo ambapo unaweza kufanya makubwa Kwa dhana ambazo zinetuzunguka. Kwa mfano ukiangalia 🌐 ChatGPT inapatikana bure 🔍 Google ni…

 • Madebe tupu huvuma

  Leo kuna kauli mbili muhimu sana ambazo nataka tuzijadili kwa ufupi tu. Kauli ya kwanza ni kauli ya wahenga watu wanaosema kwamba, madebe tupu huvuma. Na kauli ya pili ni kauli inayosema kwamba, an idle mind is a devil’s workshop. ikiwa na maana kuwa akili tupu ni karakakana ya shetani. hizi kauli zote mbili zinatusisitiza…

 • Jinsi ya kuwakomesha watu wanaokukatisha tamaa kistaraabu kabisa (Ila Utakuwa Umewakomesha)

  Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu. Kama hujawahi kukutana na watu ambao wanakukatisha tamaa, inawezekana hujawahi kuthubutu kufanya kitu cha tofauti na vile vilivyozoeleka kwenye jamii au hufikirii kwa ukubwa kabisa. Ni hivyo tu. Ila kama unafanya vitu vya tofauti, ni wazi kuwa watu wataanza kukukatisha tamaa kwenye kile unachofanya. Inawezekana watu wakakukatisha tamaa moja kwa…

 • Sahau Yote Kwenye Pesa Na Fedha Zako Ila Usisahau Haya Matano (05) Tu

  Kwenye fedha mengi ambayo unapasawa kuzingatia na kuhakikisha kwamba umeyafuata, wakati vyote vikiwa ni vya muhimu ila kuna kitu kimoja ambacho kamwe haupaswi kusahau hata siku moja. Na kitu hiki ni kwamba kamwei haupaswi kutumia pesa zaidi ya kipato chako pili haupaswi kuacha kuweka akiba tatu, hakikisha kwamba mara zote unawekeza na kuifanya fedha ikufanyie…

 • Siri Kuu Ya Mafanikio Ni Hii

  Leo nataka nikujulishe siri kuu ya mafanikio ambayo watu wengine wamekuwa hawakwambii. Unaweza kufanya yote kuhusu mafanikio lakini kama utakosea, hili uje wazi kuwa utakuwa umekosea kweli. Na kitu hiki ni kurudia makosa ambayo watu ambao  hawajafanikiwa wanafanya. Ukiona mtu ambaye hajafanikiwa, ujue kuna kitu ambacho watu waliofanikiwa wanafanya ila yeye hafanyi. Hivyo, njia pekee…

 • Kitu Kinachofanya Mabadiliko Kuwa Magumu Kwenye Biashara Yako

  Rafiki yangu salaam, Hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Siku ya leo ningependa kukwambia kitu kinachofanya mabadiliko kuwa magumu kwenye biashara yako. Kitu hiki siyo kingine bali ni kutaka wengine wabadilike huku wewe ukiwa hubadiliki. Mfano, unataka watu wawahi kufika kazini lakini wewe unachelewa. Unataka watu wafanyie kazi mabadiliko fulani lakini wewe…

 • Ninavyotunza Kumbukumbu Zangu Za Kiuandishi Zisipotee. Na Jinsi Wewe Unavyoweza Kufanya Pia

  Rafiki yangu, juzi nilikuwa naandika makala nzuri sana, nilipokuwa nakaribia kuimaliza kabisa nilibonyeza sehemu ile makala ikapotea yote. Kama unajua zoezi la uandishi lilivyo, utakubaliana nami kwamba kupoteza kazi ambayo umeandika kwa zaidi ya saa moja na zaidi ni kupoteza sana. Nilichofanya, sikukata tamaa, ilibidi nirudie kuiandika ile makala upya. Ninaposema, upya, namaanisha upya kabisa.…

 • Vitengo Vitatu Ambavyo Vipo Kwenye Kila Biashara.Hata Kwenye Biashara Yako Vipo Hata Kama Hujui. Virasimishe Sasa

  Siku za nyuma nilikuwa najiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na ukomo. Hivi huwa inakuwaje kunakuwa na vitengo kwenye biashara au taasisi. Ni nini ambacho huwa kinafanyika mpaka watu wanajua kitengo fulani na fulani vinapaswa kuwa sehemu tofauti? Biashara inapaswa kuwa imefikia ngazi gani ili kuweza kuwa na hivyo vitengo vyote? Siku ya leo ninaongelea vitengo…

 • Aina Tano (05) ya watu ambao kila mfanyabiashara anapaswa kujenga nao urafiki wa karibu

  Rafiki yangu wa ukweli salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya leo. Leo nataka kukwambia aina tano ya watu ambao kama mfanyabishara unapaswa kuanza kujenga nao urafiki mapema. Unapaswa kuanza kujenga urafiki wa namna hii mapema sana bila kujali biashara yako ni ndogo au kubwa. #1. ni wanasheria. Hawa ni watu muhimu sana kwenye…

 • Epuka Makosa Haya Matano (05) Kwenye Biashara Yako

  Rafiki yangu mfanyabiashara, Leo nataka nikuainishie MAKOSA matano ambayo wafanyabiashara Wengi hufanya. Tafadhali hakikisha kwamba unayaeouka Haya MAKOSA Kwa manufaa ya biashara Yako ya Sasa na baadaye Kosa la kwanza: kutioipa biashara Yako jina. Labda nianze Kwa kukuuliza jina biashara Yako ni lipi? Kama biashara Yako Haina jina unakosea sana. Mtoto akizaliwa anapewa jina Wewe…

 • Huu Ndiyo Muda Mzuri wa Kusema Kwamba Umefanya Mauzo Kwenye Biasshara yako

  Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii njema ya leo. Kwenye biashara kuna kitu kimoja tu ambacho watu huwa wanakosea. Na kitu hiki huwa ni kuhesabu vifaranga kabla havijatotolewa. Yaani, kuhesabu kwamba wameuza wakati bado kabisa hawajauza. Unakuta mtu anahesabu kwamba ameuza pale anapoahidiwa na mteja kwamba atakuja. Au anahesabu kwamba ameuza…

 • Aina za mazoezi Unayopaswa kuwa unafanya

  Mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kuna aina tatu ya mazoezi ambayo unapaswa kufanya kila siku, unajua ni aina zipi? Mazoezi ya mwili. Kama kukimbia, Kwa siku tenga walau musu saa Kwa ajili ya hili Mazoezi ya akili. Haya niazoezi unayafanyia Kwa kujifunza, KUSOMA VITABU na kupata mafunzo ya semina n.k Mazoezi ya kiroho.…

 • Jinsi Ya Kujilipa Mshahara Kutoka Kwenye Biashara Yako. Njia Mbili Zilizothibitishwa

  Changamoto kubwa ambayo imekuwa inawakumba wafanyabiashara wengi ni kuchanganya pesa zao na pesa za biashara. Makala ya leo, inaenda kuwa mwarobaini wa hili. Sikiliza uhusiano mkubwa uliopo kati yako wewe na biashara yako ni kwamba wewe ni mmiliki wa biashara, lakini fedha za biashara haupaswi kujimilikisha na kuzifanya kuwa za kwako. Fedha za biashara ni…

 • Kanuni Ya Miezi Sita Kwenye Biashara, Na Kwa Nini Kila MfanyaBiashara Anapaswa Kuifahamu

  Kuna kanuni ya miezi sita kwenye biashara ambayo wafanyabiashara wengi hawaifahamu. Ni kanuni muhimu ambayo kama mfanyabiashara unapaswa kuifahamu. Kutoifahamu kanuni hii kutakuponza sana Kanuni hii inasema kwamba, ukianza kufanya biashara, ndani ya miezi sita ya kuanza biashara kuna watu wengine wataanzisha biashara kama hiyo. HII kanuni inafahamika kama kanuni ya copy cat. ikimaanisha kwamba…

 • Viashiria kumi na sita (16) Kuwa Umebeba Ajira Za Watu

  Rafiki yangu mpendwa salaam, ujue mara kwa mara nimekuwa nakwambia kwamba inawezekana wewe umezaliwa kuajiri na siyo kuajiriwa. Siku ya leo ninaenda kukuonesha viashiria ishirini ambavyo vinaonesha kuwa wewe umebeba ajira za watu. Baada ya kuwa umesoma hapa sasa, kazi itabaki kwako kuhakikisha umefanyia kazi haya utakayokuwa umejifunza au la 1. Kiashiria cha kwanza kwamba…

 • UTABIRI: Kitu Kimoja Ambacho Ni Uhakika Hakitatokea Maishani Mwako

  Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendelea vyema kabisa na shughuli zako za kila siku. Siku ya leo nimekuandalia makala ya kushangaza kidogo. Na makala hii ni utabiri. Mimi syo mtu ninayeamini sana kwenye tabiri, unabii na vitu vinavyoendana na hili. Ila leo nimevutwa kukupa utabiri huu, na ninatoa utabiri huu nikiwa na uhakika kuwa…

 • Iga Ufe

  Kuna baadhi ya vitu huhitaji kuiga kwa watu wengine.  Badala yake unapaswa kuvifanya kulingana na wewe mwenyewe. Siyo kila kitu wanachofanya wengine kinaweza kukufaa na wewe pia. VIngine vinaweza kuwa sahihi kwao, lakini siyo sahihi kwako. Ni muhimu kwako kufahamu kipi ni sahihi kwako, na kuwekeza nguvu yako kubwa hapo. Kuna watu wanakopa na mshahara…

 • KIPAJI NI DHAHABU: Ila hapa kuna vitu vitano ambavyo kila mwenye kipaji anapaswa kufahamu

  Juzi kuna mtu alinifuata kikashani kwangu whatsap na kuniuliza, mbona kijana yule mwenye kipaji ameshindwa kusaidiwa?  Nilimwuliza kijana yupi? baadaye kidogo alinitumia picha za yule kijana pamoja na kazi alizofanya.  Nilitakafari hili kidogo, ila nikaja kugundua kwamba watu wenye vipaji kuna vitu vitabo muhimu ambavyo hawafahamu. Ningependa na wewe ufahamu hivi vitu, kuanzia leo hii,…

 • Kipaji chako umekiweka wapi? Umeajiriwa, umejiajiri au huna ajira?

  Dhahabu ni madini yenye thamani sana hapa duniani. Siku ya leo tarehe 29/3/2024 wakati naandika hapa, imabidi niangalie mtandaoni ili kuona bei halisi ya dhahabu sasa hivi kwenye soko la dunia. Ninachoona hapa ni kwmaba bei ya dhahabu kwenye soko la dunia siku ya leo ni kati ya dola 70,000 na dola 75,000 kwa kilo…

 • Acha Uvivu, Fanya Jambo Hili Kila Siku Bila Ya Kuacha

  Kufikiri ni jambo ambalo tunapaswa kulifanya kila siku. Wengi hudhani wanafikiri lakini kumbe siyo. Kufikiri ni kazi ambayo hatupaswi kuikwepa. Inapaswa kuwa sehemu aya maisha yetu ya kila siku. Hakuna mtu ambaye anawez akufanya hiki kitu kwa ajili yako. Kuna vitu unaweza kuwapa watu na wakafanya hivyho vitu ila huwezi kuifanya wewe. Jipe kazi ya…

X