Mazoea ni mabaya sana


Mwaka fulani wakati wa mahali la saba wanafunzi waliimba wiMbo fulani unaosema
Mazoea ni mabaya sana*2
Wimbo huu ulikuwa ni kuwaaga darasa la saba ambao walikuwa wanamalizia masomo yao na kwenda hatua inayofuata.

Sikumbuki nilikuwa darasa la ngapi kwa wakati hu[, na wimbo wenyewe siukumbuki vizuri sana, ila nakumbuka kiitikio kilikuwa kinaanza hivyo

Mazoea ni mabaya sana

na lengo kubwa la wimbo huu lilikuwa ni kuonesha kuwa la saba walishazoeleka pale shuleni, kwa hiyo kuondoka kwao kutaacha pengo. Mazoea ni mabaya sana

Leo nimeamua kuandika hivi baada ya jana kuchelewa kulala, nikitegemea nitaamka saa 1 asubuhi, 
Lakini wapi, saa nane tu usingizi umekata na hapa tayari nimeamka naandika.
Mazoea ni mabaya sana.

Juzijuzi hapa nimenunua smartwatch, nikategemea basi nitaiona ya ajabu, lakini cha kushangaza nikiikumbuka simu yangu (smartchwatch hata sina muda nayo).
Mazoea ni mabaya sana.

Ndiyo maana tunashauriwa tujenge mazoea kwenye vitu vizuri.
Siyo unajenga mazoea kwenye kubeti, utashangaa unabeti hadi mke wako kama Mwijaku.
Mazoea mabaya sana.

Mazoea mabaya sana, ila kwa upande mwingine mazoea ni mazuri sana.
Kama utaajizoesha vitu chanya.
Kama kusoma vitabu, KUWEKEZA, kufanya kazoezi.
Maana kila muda fulani wa kufanya jambo husika ukifika utajikuta unakimbia ukalifanye.
Lakini ukijizoesha kula chipsi mayai, utashangaa unanenepa wakati ulikuwa mbaumbau, eti na wewe unakuwa bonge.
Ila mazoea haya jamani


Mzee mmoja hakuwa na uvumilivu.
Msimu wa kahawa (kule uhayani kahawa ni zao lina heshima yake) ulipokuwa unafika, mibuni  ikianza kutoa maua tu, anauza maua yale kwa walanguzi ambao mara nyingi huwa wanatoa hela kidogo, ili haadaye msimu ukifika na wao waambulie kitu kwa uwekezaji wao.
Huyu mzee kila mwaka alikuwa anauza kahawa zake kwenye hii hatua
Na kila mwaka alikuwa anasema hajawahi kushika hata laki moja kwa wakati mmoja, ilihali kahawa zake tu, zingekomaa zingempa mamilioni kwa wakati mmoja. Mzee huyu ameaga dunia mwaka juzi akiwa hajawahi kushika laki moja kwa wakati mmoja kwenye mkono wake.

Mazoea haya, we acha tu.

Tena huyu mzee alizoea kujiambia kwamba sijawahi kushika laki moja. na hivyo neno lake liligeuka kuwa sheria maana imeandikwa kuwa kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kasome Marko 7:20

na wahenga wetu walishasema kitambo sana kuwa maneno huumba. ukiyatumia maneno yatakusaidia kuumbakitu kizuri au la yatakuumbia ubaya. ukiyatumia kwa mazoea (kwa kurudia rudia) akili yako inazoea kile ambacho unakuwa unajiambia.

Badala ya wewe kujiambia maneno hasi.

Anza kujiambia maneno chanya. maneno mazuri ambayo yatakusukuma mbele na kukufanya upambanie malengo na ndoto zako kubwa. Kamwe rafiki yangu usikubali kurudi nyuma wala kuyumbishwa na mtu au kitu chochote hasa kwenye kujisemea na kujinene ,maneno chanya. mara zote jinenee maneno chanya maana maneno yanaumba.

Na kwa sababu yanaumba, yakiswemwa kwa mazoea kwa muda mrefu, mwisho wa siku yanakuja kwenye uhalisia.

Ninachotaka nikusisitize wewe
Kuanzia leo
Anza kujenga mazoea chanya
Kama kusoma vitabu
Kuandika
Kunoa kipaji chko
KUWEKEZA
N.k
Mazoea ni mabaya ukiyawekeza kwenye tabia mbaya na mazuri yakiwekwa sehemu sahihi.


Asante
Mimi naitwa
Godius Rweyongeza kutoka Songambele
Tutembelee www.songambele.co.tz
Tupo Mafiga, Tenki Bovu, Morogoro, Tanzania
Simu zetu ni +255755848391 au +255684408755
Hata WhatsApp ni hizohizo.
Hatuna mbambamba wala nini




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X