Kitu Kimoja Ambacho Hakuna Mtu anaweza Kukifanya Kwa Niaba Yako


Rafiki yangu mpendwa salaam. Naamini UNAENDELE VYEMA kabia ana majukumu yako ya kila siku,  siku ya leo nimekuja kwako kukwambia kitu kimoja tu rafiki yangu. Naam, kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukifanya kwa niaba yako, Isipokuwa wewe tu ndiye unaweza kufanya hivi vitu.

Naomba kwanza ufahamu umuhimu wa kuwapa wengine majukumu. Siyo kila jukumu unaweza kulifanya mwenyewe. Baadhi ya majukumu unapaswa kuyaacha na kuwapa wengine wayafanye ili uweze kuweka nguvu zako na muda wakokwenye majukumu machache ambayo unyaweza zaidi.

Hata hivyo ifahamike kuwa siyo kila jukumu unaweza kuwapa wengine walifanye kwa niaba yako.

Moja ya jukumu ambalo huwezi kuwapa wengine walifanye kwa niaba yako ni JUKUMU LA KUONGEZA THAMANI YAKO. Thamani yako ni muhimu sana na hasa kwenye ulimwengu wa leo ambao unabadilika na unakabiriwa na mabadiliko mengi ambayo yanazidi kutokea.

Hivyo, jukumu la kuhakikisha thamani yako imeongezeka ni jukumu lako mwenyewe na wala hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya hili jukumu kwa niaba yako.

Ndiyo maana nimeandika kitabu kizima cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO, nikiwa nakuonesha hatua kwa hatua ni kwa namna gani unaweza kuongeza thamani binafsi.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba ukiongeza thamani yako, utaweza kukuza Uchumi wako binafsi pia.

Kwenye ulimwengu wa leo wanaolipwa zaidi ni wale ambao wamekuza thamani yao kwa viwango vikubwa.

Kumbe kwenye kazi au jukumu lolote ambalo unafanya. Hakikisha unapambania kitu kimoja muhimu sana rafiki yangu. Thamani yako.

Kupata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO, wasiliana nami kwa 0755848391 sasa.

Karibu sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X