Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional


Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional

Rafiki yangu mpendwa, salaam

Miongoni mwa ujuzi muhimu sana ambao unahitaji ili kufanikisha malengo Yako ya mwaka 2025 ni ujuzi wa kuipangilia wiki yako. Wiki ni ndogo sana ila usipoipangilia vizuri inapotea na ukipoteza wiki nyingi mfululizo, mwisho wa siku unakuwa umeupoteza mwaka wako. Maana mwaka una wiki 52 tu. Na kumbuka wiki yoyote unayoipoteza, hairudi hata kidogo.

Sasa ya nini uupoteze mwaka mzima wakati Kuna uwezekano mzuri tu wa kufanya makubwa kwa kuanza kitu kidogo kama kuipangilia wiki yako.

Anza wiki hii kuipangilia kila wiki yako.

Ni majukumu gani uliyonayo?

Ili kuipangilia wiki yako kiprofessional, anza kwa kujiuliza ni majukum gani yaliyombele yako kwa wiki inayofuata?

Kisha yapangilie kulingana na umuhimu. Majukumu ambayo ni ya muhimu zaidi yape kipaumbele kwanza.

Kwenye siku yako usipange vitu VINGI VYA kufanya. Ukiweza kuwa na vitu vitatu tu vinatosha, vikizidi visiwe zaidi ya sita. Hii itakusaidia kufokasi kwenye mambo machache ila utakayoyawekea NGUVU kubwa na kuyafanikisha pia.

Unavyoianza wiki yako pia, hakikisha wiki hii unapanga muda wa kujisomea vitabu. Inashangaza kuona kwamba watu wanapangilia mpaka muda wa kula ila hawapangilii muda wa kujisomea. Changamoto kubwa ni kwamba, tumbo likiwa na njaa huwa linapiga kelele. Ndiyo utasikia mtu anasema; “nina njaa“. Ila akili yako ikiwa na njaa haisemi. Ila ilipata utapiamlo wa akili, utazidi kuwa nyuma mara zote. Hivyo, fanya kadiri uwezavyo kuhakikisha kwamba, kila siku unapata muda wa kujisomea.

Pata kozi yoyote fupi. Online kuna kozi nyingi fupi. Kwenye ratiba yako weka muda wa kujifunza kozi yoyote fupi kuhusiana na eneo ambalo ungependa kulifahamu kwa undani. Inawezekana Hilo eneo tayari unalifahamy vizuri tu, lakini Kuna jambo moja au mawili unaweza kujifunza kuongezea au kutanua kile ambacho tayari unajua.

Siwezi moja kwa moja kukwambia ujifunze kozi gani, ila fahamu ya kuwa kozi za namna hii zipo nyingi. Ni juu Yako kujua wapi unahitaji KUWEKEZA NGUVU ili uwe Bora zaidi. Maeneo ya kujifunza na kupata kozi kama hizi pia ni mengi, mfano skillshare, Udemy, Coursera, learn digital with Google, na nyingine nyingi kama zinavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Pia hakikisha unaondoa vitu vyote ambavyo siyo sahihi, vitu kama mitandao ya kijamii, kuangalia video YouTube, TikTok. Kiufupi ni hivi, usiwekeze muda wako sehemu ambazo siyo sahihi, mara zote wekeza muda wako eneo sahihi ili uweze kupata matokeo sahihi.

Waangalie role models wako. Ni wazi kuwa Kuna watu ambao kwenye maisha Yako unatamani kuwa kama wao. Kwa Kila jambo unalotaka kufanya jiulize kama angekuwa [jina la role model wako] angefanya hivi? Kuna vitu VINGI unafanya ambavyo role model wako hafanyi. Viepuke.

Anza kufanyia haya kwa wiki hii, tukutane hapahapa kesho kwa ajili ya somo la jingine zuri kama hili.

Mpaka wakati mwingine.

Mimi ni Godius Rweyongeza.

Tuwasiliane 075584891

Kitu kimoja Cha ziada😁

Mwezi wa sita tunaenda kuwa na semina Babu kubwa.

Itafanyika tarehe 28 na 29 Juni. Itakuwa siku ya Jumamosi na Jumapili.

Hivyo, nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye semina hii ya kipekee rafiki yangu.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na semina jiunge kwenye kundi la semina hapa👇🏿


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X