Salaam za semina na pongezi kutoka kwa washiriki wote wa semina wa biashara na Uwekezaji 2025


Rafiki yangu mpendwa, salaam. Leo ningependa tu kukutaarifu kuwa semina yetu ya biashara na Uwekezaji imeweza kufanyika kwa kishindo kikubwa sana.

Semina hii ya pekee imefanyika tarehe 28 na 29 kwenye ukumbi wa KINGSWAY HOTEL MOROGORO MJINI

Washiriki wametoka pande mbalimbali za Dunia kuja hapa Morogoro kujifuñza maarifa sahihi ya biashara na Kila KITU kimekwenda kama kilivyokusudiwa.

Kwa Leo ningependa nikudokeze VITU 10 tu kuhusiana na semina hii

  1. Tumejifunza kuhusu Kuweka malengo binafsi na ya biashara na njia Bora ya kuyafanyia kazi. Huku tukiona kwamba njia ya kufanyiia kazi malengo kwa wiki 12 badala ya miezi 12 ni Bora zaidi.
  1. Tumejifunza kuhusu masuala yote yanayohusiana na kampuni, HATUA zote za usajili, Faida na hasara za kuwa na kampuni. Na mengine mengi mazuri kuhusu kampuni
  2. Tumejifunza kuhusu elimu ya Kodi. Hii ni elimu adimu ambayo siyo rahisi kuipata, ila sisi tumeipata. Masuala yote yanahohusiana na ulipaji wa Kodi, sasa tunayafahamu vizuri sana.
  3. Tukaona isiwe kesi, tukaendelea mbele zaidi kujifuñza namna ya KUANZISHA BIASHARA ya pamoja kama wenza. Hivi hiki kitu kinawezekana, na kama kinawezekana kivipi? Kwa maarifa tuliyoondoka nayo, tuna uhakika wa KUANZISHA BIASHARA kama wenza bila wasiwasi wowote.
  4. Tumebadilishana mawazo, tumekonekti, tumeshauriana, tumeelekezana Nini Cha kufanya kwenye biashara zetu. Kila mmoja sasa ameondoka na mwongozo kamili wa kufanyia kazi. Na Bado tutakuwa wote kwa kipindi Cha mwaka mmoja ujao tukizidi kupambana zaidi kuelekea kwenye malengo yetu.
  1. Tumejifunza kuhusu masuala ya benki, tumepata konekisheni za kibenki kutoka kwa watalaam.
  2. Lakini sote tunajua wazi kuwa wakati tunaendelea kupambana na mambo MAKUBWA na biashara ni vizuri pia kuwaandaa watoto kwa ajili ya hiyo baadaye. Tulichokifanya ni kwamba tumejifunza pia namna ya kuwaandaa.
  3. Biashara Zina misingi yake, namna ya kuziendesha, Kuweka MIFUMO imara na kujenga timu Bora. Hivi ni VITU vya Msingi sana ambavyo tumeweza kujadiliana kwa kina kwenye semina hii.
  4. Utt amis wameungana nasi kwenye semina hii kutufundisha Uwekezaji kwenye taasisi hii ya UTT AMIS. Mambo yamekuwa ni moto🔥
  5. Kuagiza mizigo china, ni KITU ambacho watu wengi wangependa kujifuñza. Tumeona hili kwa undani pia
    Kiukweli tunekuwa na siku mbili Bora sana hapa duniani. Tumezitumia vyema
    Kujitafakari,
    Kujipanga upya
    Na sasa tupo tayari kusongambele

NB: Kama hukushushiriki semina na ungependa kuendelea kupata mafunzo haya yote. Habari njema ni kwamba mafunzo haya yote yanapatikana. Tutapata video zote za mafunzo. Utalipia 50,000/- tu BEI YA OFA. Cha kufanya wasiliana NAMI kwa 0755848391 sasa Ili tuweze kuanza kufanyia kazi haya pamoja.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X