Marcus Aurelius alikuwa na utaratibu wa kuandika kwenye notebook (tuiite hivyo) kila siku. Kila siku aliandika kitu alichojifunza, iwe ni kitabuni au kutoka kwa watu aliokutana au katika vyanzo vingine.
Kile ambacho mwanzoni alikuwa anaandika kwa ajili yake, baadaye kilikuja kuonekana ni cha msaada mkubwa, mpaka maandiko yake yakakusanywa kwenye kitabu kimoja ambacho leo hii kinafahamika Kama Meditations.
Huwa napenda kuwaambia watu kuwa kwenye maisha haya kila mmoja ana jambo lake anaweza kuandika kwa ajili yake mwenyewe, familia, au hata kwa ajili ya wengine.

Naomba unisikilize rafiki yangu. Huhitaji kuwa Reginald Mengi ili uandike kitabu chako.
Inawezekana watoto wako tu kuna vitu hawajui kuhusu wewe. Sasa itakuwaje,
Hilo mimi nina uhakika nalo.
UNAPOANDIKA KITABU, unatoa nafasi ya mambo yako na historia kuendelea kujulikana kwa urahisi hata kwa miaka mingi ijayo.
Mimi nina uhakika, sambamba na mali zote utakazoacha, moja ya kitu ambacho wajukuu wako watajivunia, ni kitabu utakachokuwa umeandika. Mfano, kama mimi babu yangu angekuwa ameandika kitabu. Ningekuwa naringa sana hapa mjini. Kwanza historia yake ambayo huwa nasimuliwa nusunusu kila siku, ningeipata kwa ukamilifu bila chenga. Hili lingekuwa ni jambo zuri sana kwangu.

Mfano mdogo tu, tuchukulie historia yako. Kuna watu huwa wanafikiria kwamba ili aandike historia ya maisha yake anapaswa kuwa maarufu sana. Wengi hutolea mfano wa Mengi au Mkapa na kuonesha kwamba wanapaswa kuwa kwenye viwango hivyo ili waandike vitabu.


Wewe pia itakuwa hivyo endapo hutaandika kitabu. Wajukuu wako watakuwa wanahadithiwa historia kidogo kidogo. Vistori ambavyo havina kichwa wala miguu na hivyo hawataweza kujua historia yako kamili. Ila kama utakuwa umeiandika, wataiona kwa uzuri.

Hivyo, fikiria kuhusu kuandika kitabu cha historia ya maisha yako mara moja.
Sasa kama ungependa kupata mwongozo wa kuandika kitabu
Usimamizi
au hata kuandikiwa kitabu chako
Nitumie namba yako ya simu sasa hivi ili tuweze kuwasiliana.
Tuma namba yako ya simu kwa kujibu email hii. Asante sana