KESHO BORA INATENGENEZWA LEO


Rafiki yangu mpendwa salaam. NIchukue nafasi hii kukupongeza kwa siku hii nyingine ya kipekee. Je, wajua kuwa kesho bora inatengenezwa kwa maamuzi sahihi unayofanya siku ya leo?

Tunapoizungumzia kesho bora, siyo tu tunazungumzia mabadiliko ya kalenda, bali tunazungumzia mabadiliko ya kimaisha ambayo yatakuwa yametokea kwa upande wako.

Matokeo mazuri utakayokuwa nayo miaka kadhaa ijayo, yanaandaliwa leo. Inawezekana leo hii mambo yakawa hayako sawa kwa upande wako. Ila hilo haliondoi nguvu na umuhimu wa kusema kwamba mambo mazuri na kesho yako nzuri inaweza kuandaliwa leo hii.

Ili kujenga kesho bora, ni muhimu kufahamu kwamba huwa hakuna mafanikio ya ghafla. Mafanikio yoyote unayotaka ni mchakao ambao unapaswa kuwa nao kuufuata, hivyo basi, kesho yako bora itaweza kujengwa kama utawez akuwa na mchakato mzuri ambao unaufufta na kuufanyia kazi. NI ukweli usiopingika kuwa ili kujenga kesho bora inayomeremeta unapaswa kuanza kuiandaa leo.

Pengine unajiouliza ni kwa namna gani naweza kuiandaa kesho bora leo hii?

#1. Maamuzi bora unayofanya leo yanaweza kuwa chaChu ya kutengeneza kesho bora. Maamuzi haya yanaweza kuwa ya kuwekeza muda, nguvu, pesa uliyonayo leo, maarifa n.k

Maamuzi haya yanaweza kuwa ya kuanzisha biashara. Yanaweza kuwa maamuzi ya kuweka akiba au kufanya uwekezaji. Kwa vyovyote vile leo hii unapaswa kufanya maamuzi kuilelekea kesho bora.

Inawezekana maamuzi haya yakawa magumu sana kwako.  Inawezekana maamuzi haya yakaambatana na maumivu, ila ni ukweli usiopingika ni kwamba  usiogope kufanya maamuzi haya. Yafanye maana, usipofanya maamuzi ya kesho unayohitaji, ukakubali kulipa gharama hata kama muda mwingine inaumiza, ni ukweli usiopingika kwamba hiyo keshoa bora itabaki kuwa ndooto tu.

Inawezekana leo hii ukafanya maamuzi ya kuweka akiba, lakini wakati huu unaamua kukweka akiba, kipato chako kikawa hakitoshi. Na muda mwinigine inawezekana uhkawa unaweka akiba ila unashawikishika kutumia akiba yako. ukweli ni kuwa jipe muda na usirudi nyuma. Kubali kulala njaa siku nyingine hata kama una akiba umeiweka. Ili mwishowe, hii akiba iweze kukusaidia kwenye kufanikisha malengo ambayo umeweka.

Maamuzi bora ya kesho yako unayofanya leo yaambatanae na vitendo. Nakumbuka mara kwa mara nimekuwa nasikia watu kuwa hawana mtaji, ila unakuta mtu analalamika miaka nenda miaka rudi shida hiyohiyo. Badala ya kuchukua hatamu ya maisha na kuanza kutengeneza kesho bora ambapo watakuwa na mtaji, wanaendelea kulalamika. Ngoja ni kwambie kitu rafiki yangu, kesho bora, inajengw akwa misingi mizuri ya kuamua na kuchukua hatua.

#1. Weka malengo

Kamwe usiishi bila ya malengo, kama hutakuwa na malengo rafiki yangu kila kitu ambacho kitakuja mbele yako kinaenda kuwa ndiyo malengo yako. hivyo, ni muhimu sana kwako kuyhakikish akmwab amara zote unakuw ana malengo ambayo unayafanyi akazi na malengo haya unayasimamia kwa dhati na kwa nguvu kubwa. Nakwambia hivi kwa sababu kuna wakai baada ya kuwa umeweka malengo unaweza kujikuta unataka kuacha kuyafanyia kazi. Jikita kwenye kuyafanyia kazi malengo yako mar azote. Malengo yako  yakufanye uwe bize muda woate nbadal;a ya kuwa bize na mambo ambayo siyo sawa na siyo sahiahi kwako n aka wka maendele ya kesho yako bora.

#3.  Jifunze kila siku

Rafiki yangu, kila siku jifunze. Iko hivi, kesho bora inaandaliw akwa kuwa na maarifa sahihi pia. maarifa ni moja ya kitu cha muhimu sana kuelekea kesho bora. Hata vitabu vitakatifu kama biblia vinayapa kipaumbele. Mfalme kama Suleimani, anaonakena akiomba kupata maarifa kwanza kabla y akitu kingine chochote. Hii ndiyo kusema kwamba wewe usiipuuzie nguvu ya maarifa. Maarifa yana nguvu kubwa sana.

Isitokee siku ukasema kwamba unajua kila kitu. Kila siku kwako iwe ni siku ya kujifunza upya.

#4. Heshimu muda wako

Baada ya kuwa umepanga aratiba yakp hakikisha kwamba unaheshimu muda wako wa kazi na hufanyi mambo menine yasiyoendana na kazi uliyokusudia kufanya  kwenye ratiba yak o rasmi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X