Penye Changamoto Pana Fursa.


Ndiyo maana tunapaswa kupambana. Maisha muda mwingine yanabadilila kwa sababu Kuna changamoto, Bila ya hizi changamoto mambo MAKUBWA tunayoona Leo tusingekuwa tunayaona.

Leo ngoja nikupe Mifano ya vitu vilivyogunduliwa baada ya kuwepo kwa changamoto

1. Penicillin: Alexander Fleming aligundua penicillin, dawa ya kwanza ya antibiotic, baada ya kukutana na changamoto ya kutafuta njia ya kuzuia bakteria hatari. Ugunduzi huu umeokoa maisha ya mamilioni ya watu.

2. Internet: Mtandao wa internet ulitokana na changamoto ya mawasiliano ya haraka na rahisi kati ya wanasayansi na watafiti. Changamoto hii iliwahamasisha kuunda mfumo wa mawasiliano wa ARPANET, ambao ulizaa internet tunayojua leo.

3. Airplanes: Ndege zilivumbuliwa baada ya changamoto ya usafiri wa haraka kati ya sehemu tofauti za dunia. Ndugu wawili wanaojulikana kama Wright Brothers, walikabiliana na changamoto ya kuunda chombo kinachoweza kuruka na kudhibitiwa, na hatimaye walifaulu kutengeneza ndege ya kwanza inayofanya kazi.

4. Vaccines: Chanjo nyingi zimegunduliwa kutokana na changamoto ya kuzuia magonjwa hatari kama vile polio, ndui, na surua. Hii imekuwa moja ya njia kuu za kudhibiti na kutokomeza magonjwa mbalimbali duniani.

5. Electric Light Bulb. Thomas Edison alikabiliwa na changamoto ya kuleta mwanga wa kudumu na salama kwa watu baada ya giza kuingia. Hii ilimpelekea kugundua taa ya umeme, ambayo imebadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Kwa Nini naandika haya yote? Jibu ni Moja tu?

Changamoto, matatzizo, shida za Dunia hazitakaa ziishe. Badala yake Mimi na wewe tunapaswa kuwa na jicho la ujasiriamali mara zote.

Maana penye changamoto Pana fursa. Naomba niweke kituo ili niwahi kazini😁


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X