Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu vyanzo vingi vya kipato


Rafiki yangu mpendwa salaam, leo nataka nikwambie mambo machache kuhusu vyanzo vingi vya kipato

Kwanza hakikisha kwamba unakuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kipato. kwa vyovyote vile, usikae na chanzo kimoja tu cha kipato, mara nyingi chanzo kimoja cha kipato kikipata changamoto basi huwa unakuta kwamba watu wengi wanakutana na changamoto za kipato. Hivyo., rafiki yangu, kazi yako kubwa ambayo uanapaswa kuifanya kuanzia leo hii. Ni wewe kujiondoa kwenye lindi la kutengenea chanzo kimoja cha kipato. Badala yake kuwa na vyanzo vingi vya kipato

Mbili, kama una chanzo kimoja cha kipato. Pigana uwe navyo viwili. kama unavyo viwili, pambana uwe navyo vitatu, kama unavyo vitatu walau kuwa navyo vinne. Kiwango cha vyanzo vinne na kuendelea ni kiwango cha kuanzia walau. baada ya hapo unaweza kuendelea mbele zaidi lakini walau hakikisha unakuw na vyanzo vinne vya kipato.

Tatu, anza kulifanyia kazi hio sasa hivi rafiki yangu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X