Kwa nini ni muhimu kuhakikisha unautumia ulimwengu wa mtandao kwa manufaa


Kuna kipindi ilikuwa inaaminiwa kwamba mitandao ya kijamii na mtandao wa intaneti ni kwa ajili ya vijana, ila leo hii sote tunaona wazi kuwa mtandao wa intaneti siyo tu kwa ajili ya vijana. bali ni kwa ajili yetu sote. Kumbe mimi, wewe au mwingine yeyote anaweza kuutumia mtandao huu tena kwa manufaa makubwa.

Sote leo hii tunaona wazi kuwa tunaweza kuutumia mtandao wa intaneti kufanya mambo tofauti tofauti.

Kama bishara yako leo hii ipo mtandaoni, ni wazi kuwa kuna matokeo ambayo unapata. Kuna wateja ambao unawapata kutokana na biashara yako kuwa mtandaoni.

Na kama biashara yako haiko mtandaoni, maana yake kuna wateja unawakosa kwa sababu tu ya biashara yako kutokuwa mtandaoni.

Kitu kikubwa ambacho nataka nikusishi siku ya leo ni kwamba iweke biashara yako mtandaoni rafiki yangu. Tafuta namna ya kuhakikisha kwamba unaiweka biashara yako mtandaoni.

Njia rahisi ya kuweka biashara yako mtandaoni.

Ni moja kuhakikisha unakuwa blogu au tovuti.

Pili ni kuhakikisha unakuwa na kurasa kwenye mitandao yote muhimu ya kijamii

tatu ni kuhakikisha unakuwa unaweka maudhui ya mara kwa mara kwenye hii mitandao ya kijamii.

Nne ni kuhakikisha unakuwa na mawasiliano ambayo wateja au watakaopenda kufuatilia kazi zako zaidi wanaweza kukupata. kwa kuanzia mawasiliano haya yawe ni barua pepe, namba ya simu ya kawida na ya whatsap.

Tano USIPOE na WALA USIBOE.

Fanyia kazi kwanza haya kwa leo. Uwe na siku njema sana.

Nakutakia kila la kheri rafiki yangu wa ukweli.

Uwe na si


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X