Pesa ni nini?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa
SONGA MBELE BLOG. Imani yangu unaendelea
vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea
mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya
leo.

Pesa ni kitu ambacho kimekuwa kikizungumuziwa sana. Tofauti na raslimali nyinginezo ambazo unaweza kuzingumuzia  (ardhi, muda, maji, madini, nguvu, hewa ) pesa peke yake ndiyo raslimali ambayo haikuubwa na mwenyezi Mungu. Pesa ni matokeo ya vile vitu ambavyo vimetengenezwa na mwanadamu.

Lakini cha ajabu pesa ndiyo inachukua nafasi kubwa sana katika jamii na imepewa majina mengi sana kama hela, sarafu, fedha n.k.
Lakini pia pesa ikitumika

  • Shuleni huitwa karo
  • Mahakami huitwa dhamama
  • Kwenye ibada huitwa sadaka
  • Vyuoni huitwa bumu
  • Kwenye vyombo vya usafiri hutwa sadaka
Neno lenyewe pesa lina maana ya chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya watu.
Kadri ya mwandishi wa kitabu cha THE RICHEST MAN IN BABYLON
Soma zaidi hapa; Vitabu vitatu Vya Kusoma Kabla Mwaka Huu Haujaisha
  •  “Pesa ni kitu ambacho hutumika kupima mafanikio duniani”
  • “Pesa inakufanya uweze kufurahia huduma zote duniani”
  • “Pesa ipo ya kutosha kwa wale wanaojua na wanaofuata sheria za asili zinazolinda pesa. Unaweza ukawa unazifuata kwa kujua au kwa kutokujua”
  • “Pesa leo inaoongozwa na sheria zilezile zilizoongoza upatikanaji wa pesa pake watu walipoingia Babiloni miaka elfu sita iliyopita”
Siku zote pesa ni wazo sio kitu kinachoonekana. Pesa ni uwezekano wa kubadilisha vitu vinavyoonekana kadri ya uwezo wako. Kadri unavyozudi kufanyia kazi mawazo yako ndivyo unavyokuwa na uwezekano wa kutengeneza pesa zaidi. Ni kwa sababu hii huwezi kuichukua pesa na kukaa na kuitunza milele. Pesa haijatengenezwa kwa ajili ya kuwekwa mfukoni na kutunzwa. Kuna umuhimu mkubwa wa wewe kulielewa kwa undani somo hili
Ni kawaida sana watu kufanya kazi mwezi mmoja na wanapopata pesa huitumia ndani ya masaa machache. Kibaya zaidi watu hufanya kazi kwa zaidi ya nusu ya maisha yao na huja kuitmia pesa kwenye wikendi na sherehe tu. Baada ya muda watu hawa huanza kuhangaika na pengine kuanza na kuzunguka na vyeti kutafuta kazi nyingine.
Je kupenda pesa ni chanzo cha matatizo?
Kama tulivyoona hapo mwanzoni mwa makala hii kwamba pesa ni kati ya vitu ambavyo vinetengezwa na mwanadamu vimsaidie.
Vitu vingine ambavyo vimetengenezwa na mwanadamu ni magari, trekta, ndege, meli, kompyuta, simu intanenti
Je kuna ubaya wowote katika kompyuta ambayo imeyengenezwa na mwanadamu?
Je kuna ubaya wowote kwenye simu iliyotengezwa na mwanadamu?
Hivi vyote si vinatusaidia sana kwa kurahisisha usafiri, kulima,  kuwasiliana, na mambo mengine mengi sana.

Vivyo hivyo pesa inatusaidia kubadilishana vitu ambavyo vinaonekana wazo ambalo ni pesa. Kadri utakavyokuwa na mawazo mengi na kuyafanyia kazi ndivyo utakavyopata pesa zaidi. Mtu mwenye hotel hakuanza tu kujenga hoteli bali lilianza likiwa wazo na sasa amekifanyia kazi na limefanikiwa sana na kumuingizia pesa. Kama wazo lake asingelifanyia kazi basi pesa anayoipata kutokana na hoteli asingaipata. Kwa hiyo pesa ni wazo.
Pesa itakuwa mbaya pale itakapokuongoza wewe kwenye maisha yako
Hatupaswi kuifanya pesa kama bwana wetu. Pesa haijaetengezwa ili mwanadamu aitumikie bali imfanyie kazi. Itumie pesa kukufanyia kazi lakini isiongoze kufiri kwako na kwenda kwako
SOMA ZAIDI: Kwa nini pesa ina majina mengi


4 responses to “Pesa ni nini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X