Pesa, fedha, hela
Ikiwa kanisani au kwenye nyumba za ibada inaitwa saka
Ikiwa kwenye vyombo vya usafiri inaitwa nauli
Ikiwa shuleni kwenye vombo vya kisheria inaitwa dhamana.
Ikiwa chuoni inaitwa bumu
Ikitoka kwa mfadhili inaitwa msaada
Majina mengine ya pesa ni kodi, bili, ushuru, miamala, n.k
Huku mtaanii kwetu wanaiita maokoto, mkwanja, mshiko, mapesa n.k.
Pesa ina majina mengi kutokana na matumizi yake mengi. Pesa ni moja ya kitu ambacho inatumika kwa wingi kuliko kitu kingine chochote. Hapa duniani pesa ni ya pili kwa umuhimu, ukiachana na oksjjeni, pesa ndiyo inafuata kwa kuwa na mtumzi mengi na makubwa.
Hivyo ni wazi kuwa kitu ambacho kina matumizi mengi lazima tu kiwe na maneno mengi kulingana na watu ambavyo wanaona kwamba wanaona kinafaa.
Ni jina gani la pesa wewe unapenda kutumia?
SOMA ZAIDI: Pesa ni nini?
One response to “Kwa nini pesa ina majina mengi”
[…] Vivyo hivyo pesa inatusaidia kubadilishana vitu ambavyo vinaonekana wazo ambalo ni pesa. Kadri utakavyokuwa na mawazo mengi na kuyafanyia kazi ndivyo utakavyopata pesa zaidi. Mtu mwenye hotel hakuanza tu kujenga hoteli bali lilianza likiwa wazo na sasa amekifanyia kazi na limefanikiwa sana na kumuingizia pesa. Kama wazo lake asingelifanyia kazi basi pesa anayoipata kutokana na hoteli asingaipata. Kwa hiyo pesa ni wazo. Pesa itakuwa mbaya pale itakapokuongoza wewe kwenye maisha yako Hatupaswi kuifanya pesa kama bwana wetu. Pesa haijaetengezwa ili mwanadamu aitumikie bali imfanyie kazi. Itumie pesa kukufanyia kazi lakini isiongoze kufiri kwako na kwenda kwako SOMA ZAIDI: Kwa nini pesa ina majina mengi […]