Utavuna Ulichopanda; Hii ndiyo Sheria Kuu Ya Asili


Habari za leo rafiki na ndugu yangu, ni imani yangu unaendelea vyema katika kupiga hatua ili uweze kufikia mafanikio.
 karibu sana katika makala yangu ya leo ambapo tunaenda kujifunza sheria moja kuu ya asili.

Watu wengi wamekuwa na imani  kwamba baadhi ya mambo ambayo hutokea, basi hutokea kwa bahati tu.
Hakuna kitu (kiwe kizuri au kibaya) ambacho hutokea kwa bahati  nzuri au mbaya. Kila kitu hutokea kwa sababu kuna chanzo chake.

Ebu chukulia Juma , John na Musa wote wameajiliwa kwenye kampuni moja. Na wanafanya kazi ofisi moja. Baada ya mda Juma anapandishwa cheo na marafiki zake wanaanza kumwambia una bahati sana rafiki yetu. Hivi ni kweli Juma ana bahati? 
Ukifuatilia kwa umakini juu ya utendaji kazi wao ofisini, utagundua Juma anajituma  na kufanya kazi kwa bidii na moyo wake wote.
Je hawa marafiki zake vipi?
Utagundua marafiki zake huwa wanafanya uzembe, kazini wanapiga stori muda wa kazi, wanalalamika kwa kila jambo na hawafanyi kazi kwa moyo. ( Hawaongezi thamani kwenye kile wanachofanya).
Ungekuwa wewe ungempandisha nani cheo?
Kiukweli Juma ndiye anayefaa kupandishwa cheo. Hiyo sio bahati.

Soma zaidi hapa;Sheria Muhimu Katika Kutengeneza Pesa Na Kuwa Tajiri

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati Wa Kuanzisha Biashara

Ni mara nyingi sana nimesikia rafiki zangu wakisema watafurahi sana kama wataokota kiasi kikubwa sana cha pesa. Au kama watazawadiwa kiasi kikubwa sana cha pesa.

Ebu fuatilia kwa umakini kujua ni kitu gani kinamfanya mtu anakuwa na bahati njema au mbaya. Utagundua kuna sababu fulani zinasababisha.

Kiukweli mipango maandalizi na jinsi unavyofikria ndivyo vitakavyokuletea bahati njema.

 Hapa ndipo unakuja ukweli wa sheria kuu ya asili ambayo ni ile ya SABABU NA ATHARI. Sheria hii inasema kwamba kila ambacho kinatokea, kimesababishwa. Kila unachokiona ni athari za mambo yaliyosababishwa. Unavuna kile ulichopanda ni upande mwingine wa sheria hii. Hii ina maana kwamba upo hapo ulipo sasa kutokana na mambo uliyofanya huko nyuma. Na matokeo ya kesho yatategemea utakachofanya leo.

Hakuna kinachotokea nje ya mtu ambacho kinajenga au kuharibu maisha ya mtu. Maisha ya mtu yanajengwa au kubomolewa na kile ambacho kipo ndani yake. Na hapo tunaanzia kwenye mawazo yake. Kama yanayotokea nje ya mtu yangekuwa na nguvu, tungetegemea watu wote waliopo kwenye mazingira sawa basi maisha yao yawe sawa. Lakini hali haipo hivyo, hii ikimaanisha kwamba licha ya yale yanayotokea nje ya mtu, maamuzi hasa yapo ndani yake.

Soma zaidi hapa; Nguzo Muhimu Ya Kukusaidia Kufikia Utajiri

Maswali Matatu (03) Ya Kukusaidia Kuwa Tajiri

Usiwe na matamanio, usitegemee kupokea pasipo kutoka jasho. Usitegemee kupata mafanikio kwa bahati. Badala yake jifunze ni kwa namna gani unaweza kufikia mafanikio. Kuanza kujifunza kuhusu mafanikio ni nusu ya ya kufanikiwa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutika kwenye blogu hii 

Ili kupata makala maarumu kutoka songambele blogu ambazo hutolewa kila wiki BONYEZA HAPA NA KUJAZA FOMU

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


One response to “Utavuna Ulichopanda; Hii ndiyo Sheria Kuu Ya Asili”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X