Usijilinganishe Na Wengine


Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vinaharibu maendeleo na mafanikio ya watu ni kujilinganisha.

Hili suala naweza kusema ni tabia moja ambayo binadamu anayo na inamrudisha nyuma.
Kujilinganisha na watu sio kubaya ila  ubaya unakuja pale unapokufanya kuwa kipimo  cha maisha yako.
Pale kujilinganisha kunapokufanya kuwa mvivu wa kufikiri na  kuacha kufanya kwa kujiona wewe umepiga hatua zaidi ya wale waliokuzunguka.
Ukiona wewe ndio unafanya vizuri kwenye jamii au nyumba iliyokuzunguka basi hama hapo maana sio mahala sahihi
Grant Gardone
Usianze kujilingamisha na rafiki zako. Usianze kujilinganisha na watu waliokuzunguka. Bali wewe jua unaenda wapi na kwa mini unaenda huko unapoenda?
Kama tabia yako ni kuweka akiba basi usiache kuweka akiba kwa sababu tu rafiki yako  unayejilinganisha naye haweki.
Soma zaidi hapa; Utavuna ulichopanda
Kama unataka kulima au kuanza biashara basi anza sasa bila kusubiri. Usiige Fulani eti kisa hafanyi basi na wewe hufanyi.
Iga mfano wa miti
Mti hupandwa mbegu na huakikisha umekua na kufikia mwisho bila kuangalia miti mingine imekua kwa kiasi hicho au la! Hata kama utazungukwa na miti ambayo mifupi na midogo lakini mti utakua na kufikia ukomo wake juu kabisa
Jambo la msingi sana na la kuzingatia kila siku ni kuhakikisha umeishi siku husika. Kuhakikisha umefanya unachopaswa kufanya kwa wakati sahihi bila kuangalia kama fulani kafanya hivyo au la.
.
Jijengee utamaduni wa kufanya mambo ya muhimu sana. Ukianza siku yako andika kati ya mambo matatu mpaka sita ambayo utayafanya ndani ya siku husika. Yafanye hayo tu.
usisubiri uambiwe cha kufanya. Nenda kinyume kabisa na kile ambacho rafiki zako wanatarajia. Wakati rafiki zako wanasubiri wapewe taarifa ndio waanze. Wakati rafiki zako wanasubiri waambiwe kwamba wanapaswa kufanya Kazi fulani. Wewe anza kufanya Kazi zako kadri ulivyozipangilia na zikamilishe.
Usibiri kuambiwa wala kusimamiwa ndiyo ufanye. Fanya hata kama kiongozi wa kukusimamia hayupo
Usipende kupata zaidi.
UTAVUNA ULICHOPANDA na huwezi kupata au kula kabla ya kulipa gharama. There is no free lunch ( hakuna mlo wa bure). 
Kabla ya kupata unachohitaji lazima uwe tayari kulipa gharama. Gharama hizo sio lazima ziwe pesa bali zinaweza kuwa ni muda wako, nguvu zako au akili yako na ujuzi wako.
Usitafute njia rahisi ya kufikia sehemu nzuri ya mafanikio.
Ili kufikia mafanikio ya kudumu huna budi ya kupambana na vikwazo unavyokutana navyo kwa nguvu zako zote.  Usipende kukwepa vikwazo hata kama ni vidogo. Pambana mpaka mwisho.
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X