Vitabu Vitatu Vya Kusoma Kabla Mwaka Huu Haujaisha


Habari za leo rafiki yangu na ndugu yangu. Ni imani yangu unaendelea vyema katika safari yako ya kuelekea mafanikio.
Leo nataka nikushirikishe vitabu vitatu ambavyo vitakusaidia kupiga hatua kubwa sana ili uweze kufikia mafanikio. Vitabu hivi vimewasaidia watu wengi sana nikiwemo mimi. Naamini vitakusaidia na wewe kama utaamua kuvisoma. Jitahidi sana usome vitabu hivi kabla ya mwaka huu kuisha maana hii itakuwa hatua kubwa sana kwako kuelekea mafanikio.

Soma zaidi hapa;Faida Sita Za Kusoma Vitabu Na Makala Za Kuelimisha

 Rich Dad, Poor Dad
Hiki ni kitabu ambacho kimeandikwa na mwandishi maarufu sana duniani katika karne hii ya ishirini na moja, ambaye ni Robert kiyosaki. Kitabu hiki kinazungumzia mababa wawili wa Robert Kiyosaki, baba wake wa kwanza ni baba yake mzazi ambaye  katika kitabu hiki ndiye (poor dad) yaani baba maskini na baba wa rafiki yake ambaye katika kitabu hiki ndiye (rich dad) yaani baba tajiri. Kitabu hiki kitakupa hiki kitakupa mtazamo ya hawa mababa wawili na kuonesha ni kwa jinsi gani walipishana kikauli. Mfano wakati baba maskini anaamini “kupenda hela ni chanzo cha maovu” na baba tajiri anaamini “ukosefu wa hela ndio chanzo cba maovu”
Lakini pia utapata kujifunza sheria moja na pekee katika kutengeneza pesa. Je wataka kujua sberia hiyo ni ipi? Chukua kitabu chako hapa

Soma zaidi hapa; Yafahamu Mambo Manne Ambayo Huwezi Kujifunza Shuleni

Mbinu muhimu za kujenga mafanikio katika biashara

Think and grow rich.
Hiki ni kitabu ambacho pia kimeandikwa na mwandishi maarufu sana duniani ambaye ni  Napoleon Hill.
Kitabu hiki kitakupa mbinu kumi na tatu za kufikia mafanikio na kuwa tajiri. Utapata kujua kwamba kila kitu  huanza na wazo. Lakini uwepo wa wazo tu bila kuliweka katika katika matendo hakuwezi kuleta mafanikio. Wazo lako lazima uliweke katika matendo
Utajifunza mbinu za kuwa tajiri na kufikia mafanikio
Je mbinu hizi ni zipi? Usikose kuchukua kitabu chako hapa

Soma zaidi hapa;  Mbinu za kukusaidia kufikia ndoto zako kabla mwaka haujaisha

Jinsi ya Kuepuka Kujiua Mwenyewe Kiakili

The richest man in Babylon
Hiki ni kitabu ambacho mbinu za na namna ya kuweza kufikia mafanikio. Kitakushauri mbinu gani unaweza kuzitumia kuanzisha biashara ndogo na kuzifanya kuwa kubwa sana.  Kitabu hiki kimeandikwa na George S Clason
Ili ukipate mwenyewe bonyeza hapa

Soma zaidi hapa; Siri ya Babiloni Kuwa Mji Tajiri Kuliko Yote Duniani

Hili Ni Jambo La Pekee Ambalo Huwezi Kuliepuka

Asante zana kwa kusoma makala ya leo ni vyema sana ukachukua hatua kwa kujiapatia nakala yako kwenye simua au kompyuta yako. Utaweza kupata maarifa makubwa sana. Ambayo nina uhakika yatakukwamua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hiiIli kupata makala maarumu kutoka SONGA MBELE BLOG 
BONYEZA HAPA

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


3 responses to “Vitabu Vitatu Vya Kusoma Kabla Mwaka Huu Haujaisha”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X