Ujumbe Muhimu Kwa Wahitimu Wa Kidato Cha Sita


Habari za leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. Karibu sana katika makala yetu ya leo.

Makala ya leo imebeba ujumbe muhimu sana kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu.

Kwanza nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kupiga hatua kubwa sana ya kimasomo mpaka hapo mlipofikia.

Ni hatua kubwa ambayo watu wengi sana wamekuwa wakipigana kuipata, hatimaye walioipata ni wachache sana ukiwemo wewe. Hongera sana Rafiki yangu.

Pili ni kwamba baada ya wewe kuhitimu sasa umeondokana na utoto, wewe sio tena mtu ambaye anapaswa kukaa na kuanza kuwategemea wazazi kama ambavyo ulikuwa umezoea,

Bali huu ndio muda wako kubadilika na kuanza kufikiri kwa namna ya tofauti. Zama za sasa zimebadilika na wewe unahitaji kubadilika.

Najua ndani ya kipindi hiki utakuwa na muda mwingi sana wa kuwa mtandaoni facebook,wasapu, twitter, instagram na mitandao mingine mingi sana, kadri wewe utakavyojisikia.

Utapata Uhuru wa kuweka picha mtandaoni kadri utakavyojisikia maana unao uhuru wote wa kutumia simu, lakini pia muda unao wa kutosha na hakuna masomo ambayo yamekubana kwa namna yoyote ile. Labda kama utaamua kusoma kozi za ziada kama kompyuta, ambazo na zenyewe bado hazikubani sana kama ambavyo ulikuwa shuleni.

Soma zaidi hapa; KWA NINI MAISHA YAKO UMEYAWEKA MTANDAONI.

USHAURI.

Kwa muda huu ambao utakuwa nyumbani kuna mambo kadha wa  kadha ambayo unaweza kuyafanya yakakuinua na kukufanya uwe mtu wa tofauti na kukufikisha katika hatua ya kuanza kuingiza kipato. Hivyo ni uamuzi wako kuyachukua hapa na kuanza kuyafanyia kazi.

1. SOMA VITABU
hee!! Najua nitakuwa nimekuchanganya hapa. Maana ni juzi tu umemaliza kupambana na masomo ukiwa unajichimbia kusoma ( msuli mrefu) sasa unaambiwa tena soma.

Ndio ninaposema soma namaanisha soma, ila kwa sasa sio kusoma kule ambako umezoea bali ni kusoma kwa namna ya tofauti.

Hapa simaanishi kusoma ili upewe maksi darasani au kusoma ili ufanye mtihani. Huku ni kusoma kwa ajili yako binafsi kujiongezea maarifa na kujikuza kiakili.

Katika kusoma huku hakuna mtu ambaye atakupatia kazi ya kufanyia nyumbani (home work) wala hakuna zoezi. Unasoma kwa hiari na kwa faida yako.

Na kazi ya kufanyia nyumbani (homework) unajipa mwenyewe.

Soma zaidi: VITABU VITATU VYA KUSOMA KABLA MWAKA HUU HAUJAISHA

Kwa nini kusoma!
Najua hapa utakuwa unajiuliza kwa nini unazumuzia kuhusu kusoma na sio kitu kingine.

Zama zimebadilika, maisha yamebadilika, Ajira hatarini kumbe na wewe unahitaji kubadilika. Tupo katika zama ambazo mtu ambaye ana taarifa sahihi na anazitoa kwa wakati sahihi ndiye anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kutengeneza pesa.

Lakini zama za sasa zimejaa taarifa nyingi sana ambazo zinawekwa mitandaoni. Katika mitandao kama facebook,instagram nyingine. Taarifa zinazowekwa kwa SAA moja tu ni nyingi sana. Kumbe unahitaji kuwa mtu wa kuchagua aina ya vitu ambavyo unapaswa kusoma.
.
Lakini pia dunia ya sasa  inabadilika kwa kasi kubwa sana. Kiasi kwamba Maarifa ambavyo unayo leo hii kama hutaongezea Maarifa mengine ya ziada yatakuwa yamepitwa na wakati, yaani maarifa yako yatakuwa hayana kazi tena na utaonekana mzee sana kulingana na kile utakachokuwa unakifahamu.

Hahah! Huamini.
Ebu ngoja nikupe mfano mdogo sana,
Unaikumbuka simu janja (smartphone) ambayo ilikuwa habari ya mjini kipindi unaenda kidato cha tano? Bila shaka utakuwa unaikumbuka. Je, leo hii hiyo simu bado ni habari ya mjini? Bila shaka utakuwa unajua kwamba kwa sasa kwamba zipo simu nyingine sokoni bora zaidi ya ile ya mwanzo. Sasa kwa nini hiyo simu hiyo sasa hivi hasifiki tena.

Jibu ni rahisi sana. Ni kwamba umepitwa na wakati. Maarifa yaliyotumika kuitengeneza sasa yamepitwa, watu wengine wameibuka na Maarifa mengine na kuna na kitu kipya, kitu ambacho kina nguvu sana zaidi ya Kile cha mwanzo ndio maana unaona simu nyingine inafanya vizuri zaidi ya nyingine.

Hivyo hivyo ndivyo ilivyo kitu ambacho unakijua leo hii, baada ya miaka miwili kutoka sasa kitakuwa hakina maana.

Je nisome vitu gani?

Najua utakuwa unauliza swali hilo, hapa kuna baadhi ya vitu ambavyo unaweza kuvisoma kwa ajili ya faida yako

>>>>kwanza kabisa ni kitu ambacho  unataka kwenda kusomea chuo. Najua kuna kitu ambacho unapenda kwenda kusomea ukienda chuo. Unapenda kuwa mwalimu, mwanasheria, daktari, mwandisi n.k.

Hivi ushakaa kujiuliza na kufuatilia  walimu, madaktari, wanasheria, wahandisi ni watu wa aina gani?

Je,  ushajiuliza mazingira wanayofanyia kazi yanafananaje?
Ushajiuliza changamoto gani wanapitia?
Je unawajua watu ambao wamefanya vizuri katika sekta hiyo ambayo unaenda kusomea? Kama unawajua, wamewezaje? Kama huwajui umesubiri nini? Je, unajua kozi ambayo utaisoma itakusaidia nini?

Chukua muda ujiulize maswali kama hayo na uyapatie majibu haswa. Maana huu ndio muda wa kufanya hivyo

>>>>; pili ni vitabu vya ujasiriamali na biashara na kuhamasisha.

Najua unapenda kuishi maisha ya kitajiri, yenye furaha, amani, ukiwa una uhakika wa pesa kwamba ipo. Hapo utahitaji usome baadhi ya vitabu vinavyohusiana na mambo hayo.

Hata kama CHUO huendi kusoma Biashara. Unahitaji kuishi katika ulimwengu unaobadilika kwa namna ya kubadilika. Wewe sio wa kwanza kuishi hapa duniani, hivyo unahitaji kutambua kwamba Moja kati ya vitu vingi ambavyo unaenda kufanya Kuna watu ambao wamewahi kuvifanya kuwa tayari kujifunza kutoka kwao.

Chukua muda kujifunza kutoka kwa watu hawa.

Soma zaidi: Edius Katamugora Afunguka Mazito Kuhusu Kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.

2. AMSHA VIPAJI VYAKO.
je wewe una kipaji gani? Ni kitu gani ambacho hupendi ipite siku bila ya wewe kukishughulikia!

Ni kitu gani ambacho watu huwa wanaamini wewe unakifanya kwa ubora zaidi kuliko watu wengine?

Ni kitu gani ambacho watu huwa wanakuja kukuomba msaada uwasaidie?

Ni kitu gani ambacho kama hutakuwepo siku hiyo hakifanyiki vizuri?

Kitafute hicho maana ni sehemu ya kipaji chako. KAMA UNA SHIDA KATIKA KUGUNDUA KIPAJI CHAKO TUWASILIANE 068 408 755 (SIMU/WASAPU AU SMS), ili uweze kujipatia nakala ya kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU.

Huu ndio muda wako kuamsha vipaji vyako na kuanza kuvitumia kwa faida yako mwenyewe lakini pia faida ya wale ambao wamekuzunguka.

Ubora ni kwamba wewe umezaliwa na zaidi ya vipaji 750 hivyo ni juu yako kuamua kuamusha vipaji fulani na kuvitumia sasa.

SOMA ZAIDI: Nawezaje kupata vitabu Vya Godius Rweyongeza?

3. MITANDAO YA KIJAMII.
unahitaji kuwa na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. Usimezwe na mitandao hii maana mitandao ipo kwa ajili yako sio kwamba  wewe upo kwa ajili ya mitandao. Unapaswa kuwa na kiasi, katika matumizi ya hii mitandao, fuatilia vitu sahihi kwa wakati sahihi.

Sio kila kinachowekwa mtandaoni kinakufaa. Chagua vitu sahihi vya kuwa unafuatilia. Maisha yako usiyaweke mtandaoni. Sio kila picha inakufaa wewe kuiangalia, sio kila kideo lazima ukiangalie, sio lazima kila ujumbe unaoupata umtumie na mwenzako. Kuwa na kiasi. Sio lazima kila ujumbe uusome na uupigie kura ( comment).

4. UJUZI
Tupo katika dunia ambavyo inathamini sana ujuzi zaidi ya inavyothamini elimu uliyonayo. Ujuzi ulio nao leo hii ndio msingi mkubwa sana katika kukufanya uzidi kung’aa zaidi. Watu wenye ujuzi ndio watu ambao wameishikilia dunia katika fani mbali mbali. Kama michezo ( Mpira wa miguu, ndondi, riadha,) ujuzi wa uandishi, ujuzi wa uongozi.

Kuna ujuzi ambao unahitaji kuukuza. Kuna ujuzi ambao hauna sasa hivi ila unahitaji kujifunza huo na kuwa nao. Usikubaki hata kidogo upite katika dunia hii bila kuwa na ujuzi wowote ule. Ujuzi wako ndio utakufanya ule mema ya nchi

5. ANZISHA BLOGU
Blogu ni sehemu au mahali ambapo utakuwa unaweka vitu mbali mbali unavyojifunza na kuwashirikisha watu wengine ambao wanapenda kufuatilia vitu kama vya kwako.

Badala ya kukaa katika mitandao ya kijamii ukipoteza muda kwa kupigia kura picha na video ambazo hata wewe huwezi kufaidika anzisha blogu yako ambayo unaweza kuitumia kwa manufaa, hatimaye ukaanza kutengeneza kipato kwa kutumia blogu yako.

Zama tulizopo ni zama ambazo kila mtu anahutaji kuwa na blogu yake. Sasa hivi kila mtu akipata shida, kitu cha kwanza anakimbilia kwenye mtandao na kufungua Google ili aulize swali lake. Kumbe kama watu wataingia google na kutafuta kitu. Google ikawaleta kwenye blogu yako, utakuwa katika hatua muhimu ya kutengeneza pesa.

Ili kuweza kujua zaidi kuhusu unavyoweza kupata pesa kwa kutumia mtandao tuwasiliane. 0755848391 (wasapu tu)

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X