Moja ni kianzio kukubwa sana cha kila kitu. Hatuwezi kuzungumzia mafanikio katika sekta yoyote ambayo hayakuanza na moja.
Profesa mkubwa sana wa hesabu ukimuuliza siku ya kwanza alipoenda shuleni alijifunza nini? Atakwambia alianza kufundishwa moja. Au ukimuuliza profesa wa kiswahili amabaye anajua karbia robo tatu ya maneno ya kiswahili na ukimuuliza alianza kuyafahamu maneno mangapi? Atakwambia nilianza kulifahamu neno moja.
ANZA NA MOJA
Ukiongea na mhandisi ambaye ambaye amejenga nyumba ya ghorofa 17 na kumuuliza kwamba aliwezaje kujenga nyumba yenye ghorofa 17 atakwambia alianza na kuweka tofali moja.
ANZA NA MOJA
Ukiongea na Bide mwanzilishi na mwendeshaji wa blogu ya BIDEISM na kumuuliza unawezaje kuandika makala nzuri kwenye blogu yako atakwambia huwa naanza na neno moja
ANZA NA MOJA.
Soma zaidi hapa; kama hawa wameweza kwa nini wewe usiweze
Kumbe kila hatua katikamaisha huanza na moja. Kila kitu kizuri ambacho tunakiona au mafanikio mazuri ambayo tunaona yamefikiwa na watu maarufu sana wote walianza na moja.
Usiogope kuanza kuanza na moja hata katika michezo wanariadha huanza na moja.
Kumbe mpaka hapo tunaweza kusema kwamba kila kitu kilichofikia mafanikio huanza na moja.
Wakati tunaanza na moja tukumbuke kwamba vitu vyote hapa duniani vinaendana na sheria ya asili ya kichocheo na matokeo. Ambapo kanuni hii inasema kwamba nguvu unayoiwekeza ndiyo itakayoleta matokeo fulani
Kichocheo kizuri huleta matokeo mazuri na kichocheo kibaya huleta matokeo mabaya.
Nguvu tutakayoiweka italeta mayokeo sawa kagika maisha.
Kama tutakuwa wenye furaha basi wagu watakuja kwetu wakiwa wenye furaha (kichocheo kizuri huleta matokeo mazuri)
Kama tutakuwa watu wa kulalamika watu watakuja kwetu wakilalamika. (Kichocheo kibaya huleta matokeo mabaya)
Soma zaidi hapa; niambie rafiki zako nikwambie tabia zako.
Upandea wa pili wa sheria hii unaitwa utavuna ulichopanda.
Kwa hiyo ni muhimu kuweka kichocheo ili uweze kipata matokeo bora ili uweze kuanza na moja iliyo bora na ambayo itakuleta kwenye matokeo yaliyobora
Hakuna kitu kitakuzuia kufikia mafanikio kamautaweka kichocheo kilicho bora
Badilika sasa
Anza na moja
Anza sasa
Muda ni sasa
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Kujiunga na kikundi cha wasapu cha SONGA MBELE BONYEZA HAPA
One response to “Anza Na Moja”
[…] Kwa sababu mitandao hii ina tabia ya kupoteza baadhi ya kumbukumbu. Leo hii nilimwambia unioneshe kitu ulichoweka mtandaoni mwaka 2017. Huwezi kukiona, ukiniuliza Mimi kwamba nikuoneshe kitu nikichoweka kwenye blog mwaka 2017, nakwambia BONYEZA HAPA […]