JINSI YA KUANZISHA BLOG


Habari ya leo rafiki yangu. Siku ya leo ningependa kukuelezea ni kwa namna gani unaweza kufungua blog.

Kwanza labda nianze kwa kusema kwamba ulimwengu wa sasa hivi umebadilika. Kwenye ulimwengu wa leo mtu anapokuwa na wazo, au dukuduku sehemu ya kwanza kabisa anapokimbilia ni mtandaoni kutafuta kitu hicho.

Hiki kitu kimejenga utagemezi kwa watu, maana watu hawawezi kuishi tena bila mtandao. Na hizi taarifa za mtandaoni ambazo tunatafuta kila siku, zinawekwa na watu. Hazishuki kutoka mbinguni na wala haziwekwi na roboti (japo zipo baadhi zinazowekwa na roboti)

Usije ukafiri kwamba kuna watu wa aina fulani tu, ambao ndio wamebarikiwa kuweka vitu mtandaoni, na wengine hawajabarikiwa. Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kila mtu kabarikiwa kwa namna yake.
Kwa hiyo na wewe huwezi kukosa kitu cha kuweka mtandaoni.

Ni sifa gani napaswa kuwa nazo ili kiandike na kuweka vitu vyangu mtandaoni?

Kama wewe una ujuzi fulani, basi ujue kabisa kuwa una sifa za kukuwezesha kuweka vitu mtandaoni.

Kama wewe unapenda kufuatilia baadhi ya vitu kwa kina, labda kufanya utafiti au kujifunza. Ujue kabisa kuwa una sifa za kukuwezesha vitu mtandaoni.

Kwa hiyo kiufupi, elimu yako, ujuzi wako, udadisi wako, Ubunifu wako, kipaji chako, n.k. vinapaswa kuwekwa mtandaoni.

Je, niweke vitu vyangu mtandaoni kwa njia gani?
Mtandao umekuja na fursa nyingi. Unaweza kutumia njia ya sauti kufikisha ujumbe wako (podcast)
Unaweza kutumia njia ya video kufikisha ujumbe wako
Unaweza kutumia njia ya maandishi (Makala)
Unaweza kutumia njia ya michoro na picha

Furaha unayoipata kwa kujua kuwa na wewe unaweza kuweka vitu vyako mtandaoni

Kwa hiyo njia zipo nyingi, nyingi sana.

Ni eneo gani sasa naweza kuweka kitu changu nilichoandaa?
Kwanza kabisa ningependa ufahamu maeneo matano ambayo watanzania wanapenda kutembelea. Yaani, mitandao maarufu hala nchini. Hizi takwimu zinatolewa na mtandao wa Alexa na zinaweza kukusaidia kujua wapi walipo watanzania wengi ili uwawekee vitu vyako huko.

Mtandao wa kwanza kwa kutembelewa ni GOOGLE
Wa pili ni YOUTUBE
Wa Tatu ni Facebook
Wa nne
Na wa tano

Orodha ya mitandao mingine inayitembelewa zaidi unaweza kuiona hapa chini kwenye picha

Mitandao inayotembelewa zaidi nchini Tanzania

Imekuwepo mitandao ya kijamii kadha wa kadha ambayo watu wamekuwa wakiikimbikia na kuitumia kama Facebook, twitter, Instagram. Hii mitandao iko vizuri na imerahisisha Mambo mengi linapokuja suala zima la mawasiliano.

Ila kama una mpango wa kuweka mawazo yako mtandaoni katika namna ambayo itadumu kwa kipindi kirefu. Basi hii mitandao ya kijamii haifai. Mitandao ya kijamii ina watu ambao wanaweza kusoma au kufuatilia kazi zako. Ila kudumu ya wewe kuweka taairfa zako.

Lakini pia mpangilio wake ni ule ambao unatoa taarifa mpya kwanza huku za zamani zikiwa hazipewi kipaumbele. Breaking news, ndizo zinakaa juu.


Na umiliki mtandao uko wa MTU mwingine. Wewe unaysoma hapa najua haumiliki twitter labda kama wewe ni Elon Musk,
Haumiliki Facebook wala WhatsApp labda kama wewe ni Mark Zuck.

Ndio maana unahitaji kuwa na kitu Cha kwako, nafasi yako mtandaoni ambayo unazomi Na sehemu ya kuanzia ni kwenye blog.

JINSI YA KUTENGENEZA BLOGU

Kuna aina mbili za blogu. Blogu za bure na za kulipia.

Blogu za bure pia zipo za aina mbili

  1. WordPress (mfano wa blogu hii unaweza kuwa ni (jinalako.wordpresa.com)
  2. Blogger mfano wa blogu ya Aina hii, unaweza kuwa ni (jinalako.blogspot.com)
  3. Blog za bure, hauzimiliki wewe moja kwa moja. Zinakuwa chini ya kampuni uliyofungulia, na waweza kuifunga muda wowote wakitaka. Ila kwa mtu yeyote anayeanza, anaweza kuanza na blogu za bure.

Blog za kulipia kwa upande mwingine zinakuhitaji utoe fedha mfukoni ili kutengeneza blog. Na ukishaitengwneza inakuwa ya kwako na wewe ndiye unakuwa mmiliki halali. Yaani, tuseme unakuwa na sehemu yako mtandaoni. Kaa ambavyo google wana sehemu yao au Facebook wana sehemu yao.

Na wewe utakuwa na sehemu yako mfano jinnalako.com au jinalako.co.tz

Mpaka haponina uhakika utakuwa umepata kujifunza mengi. Kama utataka kufungua blogu ya bure Basi tembelea

ukikwama utaniambia

Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


9 responses to “JINSI YA KUANZISHA BLOG”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X