Kwa Nini Maisha Yako Umeyaweka Mtandaoni?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu

Leo tunaeda kuona ni kwa namna gani maisha yako unayaweka mtandaoni.

Ukiamka kitu cha kwanza unachokifanya ni kuchukua simu janja na kufungukua data ili kuangakia kitu gani kinaendelea mtandaoni.
Unataka kuona picha yako uliyoweka mtandaoni watu wameweka maoni gani kwenye hiyo picha au
Unataka kuangalia maoni uliyoweka kwenye picha ya rafiki yako amekujibu nini?
Kwa nini maisha yako umeyaweka mtandaoni?

Baada ya hapo unaanza kutembelea kurasa za facebook ulizozipenda kuangalia kitu gani kinaendelea. Kwa bahati mbaya sana kurasa ulizozipenda hakuna kurasa inayoelimisha hata moja. Unaishia kupata habari hasi, ambazo zinakufanya kuianza siku yako kwa mashaka.
Binafsi naona huu ni kama umeuza maisha yako kwenye mtandao.

Ukiingia wasapu kwenye makundi yako kama tisa hivi lakini bado mambo ni yaleyale, hakuna kundi hata moja linalokupa uhakika wa leo au kesho. Unaishia kuona picha za ajali iliyotokea sehemu fulani, mwizi aliyeuawa na polisi, mafuriko yaliyotokea mahali, maandamano yanayoendelea taifa fulani.

Tena kabla ya kuanza kufanya kazi yako ya siku husika unapiga picha na kuiweka mtandaoni na unaandika kuonesha kwamba umeamka, baadae ukitaka kusafiri picha umeweka mtandaoni
Ukikutana na rafiki yako picha umeweka mtandaoni,
Ukipata kifungua kinywa hiyo ni picha nyingine umeweka mtandaoni.
Watu wasipoweka maoni kwenye picha yako basi unajisikia vibaya
Kwa nini maisha yako umeyaweka mtandaoni?

Yote haya kwa pamoja yanakujengea hali ya kuiona dunia kuwa sehemu mbaya sana ya kuishi na hivyo unaianza siku yako kwa kuingiza mambo hasi kama hayo ambayo tayari hayakupi matumaini.
Tabia hii rafiki yangu nisingependa usafiri nayo 2017 maana itakufanya usiweze kufikia malengo yako kwa asilimia mia moja mwaka huu 2017.

Mwaka huu sio mwaka wa kufanya utani rafiki na lazima ujiambie hilo kila siku. Huu sio mwaka wa utani hasa kama unataka kufanya mapinduzi makubwa sana mwaka huu. Binafsi siku hizi 365 nimeziita SIKU 365 ZA KAZI.

Nifanyeje sasa?

Sehemu ya I

Nashauri kila asubuhi ukiamka ufanye yafuatayo;
1. Chukua daftari au sehemu ulipoandika malengo yako na uyasome kwa umakini sana.

2.Jiulize je, nitafanya nini kuibadilisha leo?

3. Nitafanya nini kuwasaidia watu wa sehemu hii ya dunia nilipo?

Soma zaidi hapa; Utavuna ulichopanda

4. Je, nawezaje kupanua biashara yangu?

5. Andika mambo sita ambayo unaenda kufanya siku ya leo yapange kadri ya kiapaumbele ambavyo utaanza kuyafanya moja baada ya jingine.

Soma zaidi hapa; Hiki ndicho chakula ambacho kila mmoja anakihitaji

Anza sasa

Sehemu ya II
Je, wajua kwamba mambo unayoingiza akilini mwako saa moja baada ya kuamka ndiyo yanayokuongoza ndani ya siju yako nzima. Jiepushe na habari ambazo hazielimishi, jiepushe na makundi ambayo hayaelimishi bali yanakujengea mtazamo wa kuiona dunia mbaya tangu dakika ya kwanza unapoamka .

1. Jiunge na makundi yanayoelimisha kama songambele

2. Penda kurasa zinazoelimisha kama SONGA MBELE.

3. Usifuatilie maisha ya watu wengine. Jifuatilie wewe mwenyewe maana wewe ndiwe unayejua unatoka wapi, unaelekea wapi? Usijikwamishe njiani. Hakikisha unafika unapotaka kufika , usikubali kujikwamisha au kumkwamishwa  na mtu yeyoye.

4. Wekeza katika muda.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Kupata kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA BONYEZA HAPA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asaante


BIDEISM BLOG



3 responses to “Kwa Nini Maisha Yako Umeyaweka Mtandaoni?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X