Mafanikio Ya Mwaka Mzima Yanaletwa Na Nini?


Habari zaa leo rafiki na ndug msomaji wa blog  yako ya pendwa SONGA MBELE BLOG imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kufikia mafanikio karibu sana katika makala ya leo.

Ni kawaida sana kwamba kila mwanzoni mwa mwaka watu huweka malengo mazuri kwa ajiri ya mashirika makampuni na  malengo binafsi pamoja na malengo ya familia.

Malengo haya mara nyingi sana huwa yameandikwa kwenye daftari au karatasi maalum au wengine hawajaandika lakini wanajua kwamba wanataka nini kufikia mwishoni mwa mwaka. Utekelezaji wa malengo haya huanza  mara moja mwanzoni mwa mwaka lakini mara nyingi kadri siku zinvyosogea ndivyo watu wanavyozidi kukata tamaa na na kuona kama mafanikio yanachelewa na muda mwingine kuacha kabisa kufuata malengo  yao ambayo wameyaweka na hivyo kuanza kufanya kazi bila ya kufuata malengo au bila malengo maalumu. (Wanakata tamaa)

Inasikitisha sana kufikia mwishoni mwa mwaka kukuta waliokuwa wameandika malengo mwanzoni mwa mwaka hawakumbuki hata yale malengo waliyokuwa wameandika mwanzoni mwa mwaka yako wapi. Wengine hawakumbuki hata kama walikuwa wameandika malengo yao mwanzoni mwa mwaka.

Hii ni hatari sana kwa sababu sio tu kwa sababu mtu anajikuta akiishi bila malengo kwa muda mrefu bali hata mambo makubwa ambayo angepaswa kufikia ndani ya mwaka husika anayapoteza.

Sasa kwa leo tuangalie ni kwa jinsi gani matokeo ya mwaka mzima yanatokea ili baada ya hapa tuanze kufanya kazi ili kufikia katika hatua ambayo tungependa kufikia kimafanikio ndani ya mwaka huu.

Muda mwingine yawezekana mafanikio yakaonekana yako mbali, yawezekana inaonekana hatua tunayopiga ni ndogo sana kulingana na kile ambacho tungependa kukifikia. Na hivyo kutufanya tukate tamaa au tuamue kurudia tabia zetu za kawaida tulizokuwa nazo

Mwaka umeundwa na miezi 12, wiki 52 na kila wiki ina siku saba zenye saa 24 kila moja. Mafanikio ya mtu, shirika au kampuni hayawezi kutokea kwa siku moja tu mwishoni mwa mwaka bali ni mafanikio yatatokea kutokana na utumiaji vizuri wa siku ambazo ndizo zinaunda mwaka. Ukifanya vizuri ndani ya siku husika kuelekea lengo lako upo katika njia nzuri ya kufanikisha lengo la mwaka.

Kumbuka mwaka huu hauna kitu chochote kilichobadilika isipokuwa namba ya mwisho ya mwaka. Mambo mengine yako vile vile mpka pale utakapobadilika

Soma zaidi hapa; Mambo matano ya kuzingatia kabla kabla ya kuanza jambo lolote.

Maisha yaliyofanikiwa sio zaidi ya siku nyingi ambazo zimefanikiwa kwa pamoja na kama utataka ufikie lengo lako mwaka huu itakupasa utumie muda fulani kila siku ili uweze kufikia lengo lako husika.

1. Anza kufanya
Mara nyingi sana watu tunakosa uthubutu wa kuanza kufanya, tunashindwa kuanza kufanya japo jambo dogo ambalo litatupelekea kufika sehemu fulani. Kipaji, ujuzi na maarifa uliyonayo hayawezi kufanya kazi mpaka pale utakapokuwa umeanza kuyafanyia kazi. Anza kidogo. Wahenga wanasema habahaba hujaza kibaba.
Anza sasa rafiki

Soma zaidi hapa;  mambo manne ambayo huwezi kujigunza shuleni

2. Utafanya nini leo?
Mara nyingi sana watu huwa tunajikuta tunaanza siku bila kujua tunapaswa kufanya nini ndani ya siku husika. Na hivyo kukuta siku imefikia mwisho tukiwa tumechoka na hatuoni kama tumefanya kitu. Hii ni hatari sana.

Unapoianza siku yako, andika mambo sita ya kufanya ndani ya siku husika. Yapangilie kwa jinsi ambavyo utayafanya kwa uzito wake. Anza kufanya jambo nambari moja. Hakikisha unajitahidi kulifanya kwa bidii sana, na usiache kulifanya na kwenda kwenye jukumu nambari mbili kama jukumu la kwanza bado halijakamilika

3. Kuwa na mtazamo wa siku husika.
Kila siku jioni kabla ya kulala ipitie siku yako husika kwa kuangalia mambo gani umeweza kuyafanya vizuri zaidi ndani ya siku husika. Angalia ni mambo gani ambayo unaweza kuyasogeza mbeleni ili uweze kuyafanya tena.

Jipongeze kwa mambo uliyoyafanya vuzuri. Lakini kama hayakuenda vizuri jipe muda wa kuweza kushughulika na shughuki zako kesho

Nakutakia utekelezaji mwema
Kumbuka kwamba haya mambo ukiishia kuyasoma bila ya kuyafanyia kazi basi hayataleta mabadiliko
Nakushauri sana uyafanyie kazi kuanzia sasa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


3 responses to “Mafanikio Ya Mwaka Mzima Yanaletwa Na Nini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X