Vitu vyote duniani havibaki kama vilivyo bali vinabadilika kadri ya mazingira na maeneo. Binadamu pia hajaachwa nyuma katika mabadiliko haya. Na ni mtu ambaye anabadilika kila siku katika utendaji, ukuaji na kufikiri.
Hii ni sheria ya asili yaani, kama ambavyo mti unapandwa ukiwa mbegu vivyo hivyo binadamu anahitaji kubadilika hili kuendana na mazingira.
Mabadiliko yana changamoto zake lakini bado huitaji kuyakataa bali unahitaji kuyapokea ili yaweze kukusaidia.
Wakati mti unakua ukikosa mwanga basi hausemi sasa ndio mwisho Wangu wa ukuaji. Bali mti hutafuta mwanga ulipo ili uweze kuendelea kukua na kweli hatimaye mti hukua. Kama mti unaweza kufanya hivi kwa nini wewe usiweze kufanya hivi.
Au mtoto akianza kukua na kuanza kutembea huwa anaanguka kila akijaribu, lakini bado haachi, hatimaye huweza kutembea. Lakini haishii hapo, mtoto pia huweza kukimbia, na pengine kushiriki mashindano makubwa kama Olympic na kushinda.
Je, kama angeamua kuacha kutembea siku ya kwanza baada ya kuanguka angeweza kushiriki mashindano makubwa kama haya?
Sasa kwa nini wewe ukikutana na vikwazo vidogo unaacha? Kwa nini unaogopa na kukata tamaa?
Haya ndio mambo ambavyo yanakuzuia.
1. Hutaki kulipa gharama?
Najua unashangaa gharama gani napaswa kulipa? Ndio ni gharama ya Kile ambacho unapaswa kufanya. Tukienda hotelini tunakula kwanza na baadae tunalipa. Lakini katika maisha unalipa kwanza na kabla ya kula.
Ukienda shuleni unasoma, unanunua vitabu, unalipa ada na kununua daftari ili upate elimu itakayokusaidia kufanya kazi. Hapo umelipa gharama.
Utakapoanza kulipwa kwa kutumia ujuzi wako ambao umejifunza kwa kulipa gharama basi tunasema umekula.
Mkulima akienda kulima shambani amatoa hela ya vibarua anatoa hela ya pembejeo na kuhakikisha amefanya umwagiliaji wa kutosha na hata kukinga mazao dhidi ya wadudu, anaendelea kufanya hivi mpaka wakati wa kuvuna. ( hapo tunasema analipa gharama). Baadae anapopeleka mazao sokoni kuuza hapo ndipo tunaposema anakula. Wewe ni gharama gani ambayo unapaswa kulipa na utailipa kwenye eneo gani? Ukweli ni kuwa gharama haziepukiki. Ni lazima tu uzilipe kama unataka kufanya makubwa.
2. Hauna malengo.
Kuna utafiti ulifanywa nchini marekani kwa wanafunzi wa chuo kikuu na kugundua kwamba asilimia 97.7 ya wanachuo ( wahitimu) hawakuwa na malengo. Huku asilimia 2.3 tu ndio ilikuwa na malengo.
Kuna mambo mawili ambavyo huwafanya watu wasiweke malengo.
💧uoga
Uoga huu unatokana na mambo Yale ambayo sisi huwa tunaingiza kichwani. Ukiingiza mambo chanya huleta matokeo chanya na ukiingiza mambo basi basi lazima utegemee matokeo hasi ambavyo yanaweza kujitokeza kwa mfumo wa uoga.
Baadhi ya mambo basi ambavyo yanaweza kupelekea uoga ni kama.
- Kusikiliza taarifa ya habari kwenye redio au TV asubuhi au muda wowote. Mara nyingi habari hizi huwa ni hasi lakini pia husababisha kuianza siku yetu kwa mtazamo ambao ni hasi. Hutufanya tuione dunia kama sehemu ambavyo haifai mtu kuishi.
Soma zaidi; wiki Wiki Moja Bila Habari
- #USHAURI (I) Epuka sana kusikiliza habari muda wa asubuhi maana mara nyingi unachokiingiza akilini mwako asubuhi (saa moja) baada ya kuamka. Huwa kina nguvu kubwa sana na kinaweza kukuonesha ni aina gani ya siku ambayo unaenda kuwa nayo.
- USHAURI (II) Ingiza habari chanya kila uamkapo asubuhi kutoka kwenye vyanzao chanya. Hapa nitaambatanisha baadhi ya vyanzo hivyo. Vyanzo hivyo ni kama vitabu vinavyoelimisha na kuhamasisha, blogu kama SONGA MBELE, BIDEISM, AMKA AMKA MTANZANIA, GEOFREY MWAKATIKA. Huku utapata habari chanya zitakazokusaidia kuianza siku yako kwa ubora wa hali ya juu sana.
- Aina ya marafiki ulionao
- Niliwahi kuandika makala tenye kichwa cha NIAMBIE RAFIKI ZAKO NIKWAMBIE TABIA YAKO Tabia yako ni wastani wa watu sita waliokuzunguka. Kwa hiyo kama umezungukwa na marafiki wenye mtazamo chanya juu ya maisha basi utakuwa kwenye mwelekeo bora wa maisha.
- #USHAURI (I) Chagua marafiki ambao unaendana nao kwa tabia, kwa kufikiri na kiutendaji. Wapunguze marafiki ambao wanakurudisha nyuma nakukuzuia kusonga mbele.
- USHAURI (II) Tafuta watu waliofikia mafanikio na uwaunganishe kwenye mzunguko wako kwa kuwa na washauri kuhusu kile ambacho unafanya. Hawa ndio watakaokusaidia kufika unapotaka.
Malengo ni muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya maisha.
Malengo yaliifanya Japani ikue kiuchumi.1950 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja katika uzalushaji wa nguo ndani ya miaka 10. Hivyo walianza uzalishaji. Na kweli lengo lao lilifikiwa kama ambavyo walikuwa wamepanga.Miaka ya 1960 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja wa vifaa vya chuma ndani ya miaka kumi.
Na kweli ndani ya miaka kumi Japani ilikuwa inaongoza kwenye uzalishaji wa bidhaa za Chuma.
Miaka ya 1970 Japani iliweka lengo la kuwa mzalishaji nambari moja wa bidhaa zitokanazo na wanyama ndani ya miaka 10.
Kweli ndani ya miaka kumi Japani waliweza kuwa wazalishaji nambari moja wa bidhaa zitokanazo na chuma. Na kweli waliweza
Nenda kaweke malengo.
Malengo tanafanya kazi.
Miaka ya 1980 Japani waliweka lengo la kuwa wazalishaji nambari moja la kuwa wazalishaji nambari moja wa vifaa vya umeme ndani ya miaka kumi (10). Kweli baada ya miaka hiyo waliweza, unajua kwa nini?
Sababu ni kwamba malengo yanafaya kazi.
Tatizo watu wanapoteza muda mwingi
Kupanga na kukaa kwenye vikao vya sherehe badala ya kupanga kuhusu ndoa yenyewe.
Wanatumia muda mwingi kupanga jinsi ya kupata kazi badala ya kupanga jinsi ya kutoa huduma kwa watu.
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com