.
Habari za siku ya leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za SONGAMBELE. Imani yangu umeianza siku yako kwa namna ya tofauti na unaenda kufanya kitu cha tofauti sana leo. Leo ni siku bora sana hakikisha kwamba unafanya kitu ambacho ni bora sana. Kile ambacho kinaweza kupimwa lazima kitaongezeka ubora. Hivyo hakikisha unaongeza ubora wa kazi yako ndani ya siku ya leo.
Karibu sana tuanze kusafiri na kuona kilicho ndani ya makala ya leo juu maana mbovu ambayo imetolewa na jamii yetu kwa wanachuo.
Jamii yetu imekuwa na utaratibu wa kuvipa vitu maana mbali mbali kulingana na mazingira na wakati. Maana hizi Mara nyingi tunaweza kusema kwamba zinakuwa hasi au chanya. Maana chanya zinakuwa na mchango bora na kuonesha kitu kikichomo wakati maana basi Mara nyingi zimekuwa sio za kumwinua MTU na kumtoa hapo alipo na kwenda hatua ya ziada.
Kwa kuanzia jamii yetu imekuwa inatoa maana tofauti tofauti pale inapomwona mvulana amesimamam na msichana, au wanatembea kwa pamoja. Jamii yetu Mara nyingi imekuwa ikiwachukulia kama watu ambao wanajihusisha na mapenzi. Hii sio tasfri nzuri sana hasa pale tunapokuwa tunaandaa kizazi, cha viongozi ambao hapo baadae wanakuja kukaa pamoja na kulijenga taifa.
SOMA ZAIDI HAPA; Mtoto Umleavyo, Ndivyo Akuavyo.
Jamii yetu pia imekuwa ikitoa maana kwa mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi. Maana hii mara nyingi imekuwa ya kumwinua sana na kumweka matawi ya juu sana. Imekuwa inamwona mfanyakazi kama mtu ambaye ana pesa nyingi sana. Hali hii imewafanya wafanyakazi kuishi maisha ambayo haswa hawapaswi kuishi. Hali hii imewafanya wafanyakazi kutumia zaidi ya wanavyoingiza pesa, hivyo kuzidi kutengeneza kizazi cha maskini mwaka hadi hadi mwaka.
Jamii haikuishia hapo, bado imetoa maana kwa MTU mmoja mmoja. Kila mtu kuna namna ambavyo jamii inamchukulia na muda wote mtu Huyo hategemewi kwenda kinyume au kufaya zaidi ya hapo. Unapoamua kubadilika na kufanya kwa namna ya tofauti, basi jamii itakushangaa sana na kuanza kukurudisha nyuma. Maana hizi zinazotolewa sio nzuri na ukiziendeza basi lazima utapotea.
SOMA ZAIDI; PESA NI NINI?
Kilichonishangaza zaidi ni maana ya mwanachuo. Jamii inamwona ni mtu ambaye ni msomi wa hali ya juu sana na mwenye kila aina ya uelewa. Na hii ndivyo inapaswa kuwa, ingawa sio hivyo wakati wote. Kwa hilo jamii inaweza kuwa sahihi lakini wanachuo wenyewe wakawa hawajalitambua hilo, kwa kuhakikisha wanatafuta na wanakuwa na Maarifa sahihi kwa kusoma vitabu mbalimbali. Naipongeza sana jamii yetu, kwa hilo, ila nawaomba wanachuo wajirekebishe kwa hilo. Wahakikishe wanakuwa watu wenye maatifa sahihi, ili maana inayotolewa na jamii juu yao iendane na Kile ambacho wanacho.
Hali hii imewafanya wanachuo kubweteka na kutochukua hatua kabisa za kimaisha na kuhakikisha kwamba wameweza kuvuka hatua mbalimbali na kwenda hatua za mbeleni. Wanachuo wamejikuta wakiwa hata hawataki kuchukua jembe kulima hasa pale wanapoenda kijijini kwa sababu ya maana hizo mbili ambazo zinatolewa hapo juu. Kitu ambacho kinatufanya tunazidi kuzalisha jamii ambayo haiwajibiki.
Mwandishi wa makala hii ni mwanachuo na anaamini kwamba huu ni wakati wa wanachuo kubadilika na kuanza kufikiria kwa namna ya tofauti umefika.
1. Mwandishi anaamini kwamba mwanachuo anapaswa kuwa mtu wa kuzalisha Ajira baada ya chuo na sio mtu wa kuanza kuhangaika kwa kutembea na vyeti mtaani kutafuta kazi.
SOMA ZAIDI; UJUMBE MUHIMU KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA.
2. Mwanachuo anapaswa kuwa mtu wa kutumia kipaji chake kuielimisha jamii.
3. Mwanachuo ni mtu wa kuionesha jamii na watu wengine kwamba kila mtu ana kitu ndani yake, ambacho kinamtofautisha yeye na watu wengine hapa duniani. Hivyo haifai hata kidogo sisi kutoa tafsiri kama ambavyo jamii yetu imekuwa inachukulia Bali tunapaswa kubadilika.
MAKALA NYINGINE ZINAZOHUSIANA NA HII;
One response to “Hii Ni Maana Mbaya Ya Mwanachuo Kuwahi Kutolewa”
[…] SOMA ZAIDI: · Hii Ni Maana Mbaya Ya Mwanachuo Kuwahi Kutolewa […]