Hii Ni Siri Iliyo Nyuma Ya Kauli Niko Updated!


Kuna kasumba ambayo inavuma kwa kasi sana siku hizi kutoka kwa watu kwamba wanataka kuwa UPDATED kila mara.
Nimeamua kutumia neno upadated kama lilivyo bila kupindisha ili ujumbe sahihi uweze kuwafikia watu sahihi ambao wanahusika.
Kama unaona msemo huu ni mpya kwako na hauelewi nakushauri sana uache kusoma makala hii na utafute makala nyingine ambazo utazielewa ili uweze kuedelea kusoma na kupata maarifa mengine.
Naweza  pia kukushauri kwamba utafute kazi nyingine ya kufanaya na uachane na hii maana hapa utapoteza muda wako, na siku zote muda ni mali. 
Bila kupepesa macho narudi kwenye mada yetu ya leo. Na sasa nataka kuongea na wewe ambaye  kila siku uanjidai unahitaji kuwa UPDATED .   
Una kisingizio cha kwamba unahitaji  kupata habari mpya kutoka mtandaoni kila wakati.
Hii imekuwa ni kauli mbiu ya watu wengi sana ambao wametuzunguka katika jamii zetu.
Vijana siku hizi wanakimbizana kutafuta na kununua simu mpya kila siku madukani, simu za SMARTPHONE kwa kisingizio cha kwamba wanataka kuwa UPDATED. Hii upadated hii, ambayo inazungumziwa na watu wengi sana maana yake nini?
Baada ya kufuatilia kutoka kwa vijana wengi sana ambao wamenizunguka nimegundua kwamba wanapozungumzia neno upadated wanakuwa wanamaanisha kuwa na habari mpya kila wakati kwa kuwa mtandaoni, kusikiliza redio na kuangalia televisheni.
Lakini kuna kitu ambcho mimi nilikuwa bado sijakijua ambacho ni ni hiki kitu kinaitwa STATUS  za wasapu. Kumbe siku hizi wasapu kuna status za video!!!!! Nilikuwa sijui!!!! Sasa hivi vijana wanapoteza muda mwingi sana kuhakikisha kwamba wanaangalia status hizi za wasapu ambazo zinawekwa na watu kwa kisingizio cha kwamba wanakuwa UPDATED! 
SOMA ZAIDI; Kwa Nini Maisha Yako Umeyaweka Mtandaoni
Mtu unaamka asubuhi na kufungulia redio au televisheni na kusikiliza magazeti kwa kisingizio cha kwamba unakuwa UPDATED! 
Hivi unakuwa UPDATED na mambo haya kwa kutaka kwenda wapi? Hivi unajua kwamba kwa sasa tunaishi kwenye ulimwengu ambao unatoa thamani kwa mtu ambaye maarifa sahihi na sio mtu mwenye vyeti?
Na wewe  maarifa gani sahihi unayo kama visingizio vyako ni vile vile vya kuwa UPDATED

Mwandishi LAZARO SAMWELI aliwahi kuandika katika moja ya makala yake kwamba hata MARK ZUCKERBERG hakai mtandaoni muda wote kwa kisingizio anakuwa updated.
Ndio maana tunaona kwamba kampuni ya faceebook inazidi kusonga mbele. Hii ni kwa sababu tu kwamba mhusika mkuu yupo anawezekeza na kuhakikisha kwamba anatafuta maarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi.
Ukiona facebook wanakwambia kwamba unahitaji kupakua APP mpya ambayo itakufanya uzidi kuendana na wakati sio kwamba wao muda wote walikuwa mtandaoni wanakuwa UPDATED, bali walikuwa kazini!
Rafiki yangu usipoutumia muda wako kuhakikisha kwamba unafanya kazi, ukabaki mtandaoni kwa kisingizio cha kuwa UPDATED, umepotea.
Katika kufikiria hili suala la kuwa UPADTAED, nimegundua kwamba vijana au mtu yeyote anayepoteza muda wake akiwa mtandaoni kwa kisa cha kuwa UPDATED anapoteza mambo yafuatayo!SOMA ZAIDI; Mambo Matatu Unayohitaji Ili Kufikia Ushindi

 1. MUDA,  muda ni raslimali ambayo inapokuja hairudi tena, ikipita imepita!
Hatuna tena muda ambao unaweza kujirudia rudia. Vijana wengi wamejikuta kwamba wanapoteza kwa kutafuta kuwa UPDATED badala ya kutafuta MAARIFA NA UJUZI sahihi.
Kama unaishi katika ulilmwengu wa sasa hivi ambapo uwezekano wa kupata maarifa ni mkubwa sana kuliko ambavyo imewahi kutokea ulimwengu huu na hauna ujuzi wala maarifa sahihi. Na bado unamiliki simu tu, kila wakati upo mtandaoni. Uza hiyo simu,, ukaanzishe walau mradi wa kufuga kuku.


2.     UWEZO WA KUFIKIRI: hapo zamani za kale mababu zetu hawakuwa na kitu kinaitwa kuandika wala kuchora. Taarifa zote za msingi sana walikuwa wanabaki nazo katika akili zao na kuzitunza.
Kadri hali ilivyozidi kubadilika mambo nayo yalizidi kubadililka na kila kitu kilizidi kubadilika.
Hatimaye uligunduliwa wino na mambo yakaanza kuwekwa kwenye karatasi. Uwezo wa kutunza kumbukumbu ukaanza kupungua kwa watu kwa sababu tu waliona wanaweza kukandika kila kitu kwenye karatasi au ukuta.
Hivyo hakuna mtu ambaye angejisumbua kwa kuhakikisha kwamba anatunza vitu kichwani mwake.
Japokuwa uwezo wa kutunza kumbukumbu ulipungua lakini bado uwezo wa kufikiri haukupungua, maana kuandika kunaongeza uwezo wa mtu wa kufikiri.
Baadae ilikuja mitandao ya kijamii ambayo sasa imeharibu kila kitu. Imepunguza uwezo wa kufikiri lakini pia imepunguza uwezo wa kukumbuka. Kama bado unaendelea na mambo yako hayo ya kuwa updated hili linakuhusu. Hii ni habari mbaya ambayo mimi huwa sipendi kuitioa nikiwa wa kwanza ila leo hii nimelazimika kufanya hivyo.

SOMA ZAIDI: Inawezekana kuondokana na madeni..
3.     MTAJI: kuna mashindano ya nani ana simu kali, au simu ambayo Inaonekana ya kijanja. Kwa hiyo watu wamejikuta wakinunua simu mpya kila siku ili wao waonekane ndio wajanja au watu wanaoenda na wakati. Watu hao hao ndio wanaolalamika kwamba hawana mitaji ya kwenda kuanzia biashara!!!!  
Hili ni jambo ambalo linapaswa kuongezwa kwenye maajabu saba ya dunia na kuwa ajabu la nane. Hivi wewe kijana ambaye unalalamika kwamba hauna mtaji unajua kwamba mtaji unao mkononi mwako!
Kama hujui jambo hili basi hii ndiyo habari mpya ambayo ninakupa sasa hivi. Uza simu yako ili upate mtaji wa kuanzia biashara. Hakuna haja ya wewe kuendelea kuwa mtandaoni wakati hauna hata pesa ya kununulia vocha bali unategemea kifurushi cha bure. Hakuna haja ya wewe kusema kwamba unakuwa UPDATED wakati unahangaika na mtaji. UZA SIMU UANZISHE MTAJI WA KUKU. Hakuna umuhimu wako kuwa na simu ya laki tano wakati hauna mtaji.

Mbali na kupoteza hayo mambo matatu nikagundua kwamba nguvu kazi, ambayo ingetumia muda mwingi katika kufanya kazi leo hii inazidi kupotea. Huu ndio ukweli. 

Kama lengo lako kuu ni kuwa updated endelea!


MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.
 
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba
 
1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.
 
2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.
 
3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.
 
JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.
 
Jinsi ya kulipia.
 
Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.
 
MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.
 
2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.
 
3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.
 
4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.
 
Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.
 
Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu

 
 
Ni Mimi Rafiki na kocha wako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godius
Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii


Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA 
Kujiunga kundi la wasapu la SONGA MBELE BONYEZA HAPA

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X