Maisha Ndani Ya Darasa Ni Tofauti Na Maisha Nje Ya Darasa


Nampenda sana ROBERT KIYOSAKI kwa jinsi anavyodadafua maisha ya shuleni na kuyaweka katika hali ya kawaida ya maisha.
Maisha ndani ya shule yana mfumo wake wa kuishi, mfumo ambao ni wa tofauti kabisa na maisha nje ya mfumo wa shule.
Au kiufupi tunaweza kusema kwamba maisha ya shuleni ni digrii 180 na maisha nje ya shule.
Katika shule unajifunza kusoma na kuandika, maisha yanakutaka kabisa usome na kuandika.
Wakati shuleni unafundishwa kwamba kuna milango mitano ya fahamu maisha ya mtaani yanakuhitaji utumie hiyo milango yako yote ya fahamu.
Wakati shuleni unajifunza kwamba kuna ajira maisha yenyewe yanakuajiri.
Wakati shuleni unajifunza kwamba unapaswa kuwa mtu wa watu, maisha yanakulazimisha wewe kufanya hivyo.
Kwangu mimi mwalimu mzuri ni yule anayekufundisha jinsi ya kuvua samaki sio yule ambaye anayekupa samaki.
Hivyo maisha ya mtaani ni mwalimu mzuri sana kuliko shule.
Ili kupiga hatua kubwa ambayo umekusudia kupiga utahitaji umkumbatie sana mwalimu maisha ya mtaani lakini pia mwalimu shule usimwache.
Mwalimu maisha ya kitaa anafundisha mambo mengi sana ambayo huwezi kujifunza shuleni.
Hivi hapa ni vitu vitatu ambavyo huwezi kukuta katika madarasa ya mwalimu shule lakini unaweza kuvikuta katika madarasa ya mwalimu maisha
·         UJASIRIAMALI: shule nyingi sana zimejitahidi kufundisha somo la uchumi, kwa wanafunzi wengi sana.
Na baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakihadaika kwamba unapojifunz somo la uchumi basi wewe moja kwa moja unakuwa mtu mzuri sana katika masula mazima ya uwekezaji na biashara.
Hii sio kweli. Kinachofundishwa shuleni ni mtazamo wa kupewa samaki sio mtazamo wa kuvua samaki. Hivyo ukiendelea na mtazamo huu na kuumbatia basi utakuzamisha kwenye kilindi cha maji mapana ya bahari.
Somo zima la ujasiriamali linafundishwa kwenye mfumo wa kawaida wa maisha.
Na hapa ni ndipo unahitaji kuwatafuta watu sahihi wenye maarifa sahihi ili waweze kukuhakikishia kwamba umeweza kupata kile ambacho unakihitaji kama sehemu ya ujuzi wako.
·         KUSOMA VITABU. Shuleni unajifuza jinsi ya kusoma lakini shule haikuchaguli aina ya kitabu cha kusoma.
Maisha unayotaka kuishi au kufikia yatakuonesha aina ya kitabu ambacho unapaswa kusoma. Sasa ni juu yako. Kichukue na ukisome au acha.
·         UJUZI WA KUWASILIANA. Siku hizi sio ajabu kusikia kwamba mwanafunzi amehitimu chuo na hawezi kusimama mbele ya watu na kujieleza mwenyewe kwa kutoa maoni au kile ambacho kimo ndani yake.
Rafiki yangu, kama huwezi kujieleza, basi  jua kwamba unapoteza sana na huu ni ujuzi wa muhimu sana ambao unapaswa kuhakikisha umeujenga na kuwa nao.
Kama huwezi kufikisha ujumbe wako jua kwamba kuna vitu vya msingi sana ambavyo wewe binafsi unapoteza.  Moja ya sifa ya Viongozi wote maarufu sana, ni uwezo wao wa kujiileza na kufikisha ujumbe wao kwa wahusika.
Kama mpaka sasa hivi huna ujuzi huu, hakikisha kwamba unanitumia ujumbe kupitia namba 0755848391 ili niweze kukusaidia.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X