NIMEZALIWA MSHINDI; Huu Ndio Ujuzi Ambao Hauuzwi Sokoni


Kuna vitu ambavyo unaweza kuvinunua sokoni, na kuna vitu huwezi hata siku moja kuvinunua sokoni. Kuna vitu ambavyo upatikanaji wake unakuwa mgumu wakati vitu vingine upatikanaji wake wake ni kawaida.

Wakati vitu Vingine vinakubitaji uwe na pesa,, ili uvipate vitu vingine vinahitaji juhudi yako tu ili viweze kuwepo. Vinahitaji pia muda wako ili uvipate.

Kuna ujuzi hapa ambao wewe hapo hauna. Na unazidi kupoteza muda mwingi sana kwa sababu tu ya kutokuwa na na ujuzi huu. Haujali kwamba muda ni rasilimali yako ya muhimu sana ambayo unayo hivyo hupaswi kuuchezea, bado hauweki juhudi yoyote ile ili kuhakikisha kwamba umeutafuta ujuzi huu.

Ndio ujuzi huu ni kuwa na mpangilio. Inalipa sana ukiwa na mpangilio na unajua kitu gani ni cha wapi, na kinapaswa kufanyika wapi?

Linapokuja kwenye suala la mpangilio huwa napenda kutolea mfano wa mpishi wa hoteli au mgahawa, hasa ukimwangalia muda wa chakula ukiwa unakaribia.

Huwa anafanya vitu vyake kwa mpangilio. Kila kitu ambacho huwa anagusa huwa kina maana huwa kimepangiliwa. Huwa anajua kwa nini amegusa kiungo fulani, na kila hatua ambayo Huwa anapiga huwa ina sababu zake.

Hawezi kuchukua kiungo cha kachumbari na kukiweka kwenye mboga za majani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila kitu kimepangiliwa na kina sababu.

Na wewe unapaswa kuwa na mpangilio na kujua kitu gani unapaswa kufanya na kwa nini? Sio kila hatua ambayo utapiga inakufaa bali unapaswa kupiga hatua chache na za muhimu sana.

Mpangilio ni kitu ambacho kimekuwepo tangu kuumbwa kwa dunia.

Dunia imekuwepo kutokana na kwamba kuna mpangilio.

Wewe upo hapo kwa sababu tu kwamba kuna mpangilio mkubwa sana unafanyika ndani yako. Chakula unachokula kinapangiliwa na kuwekwa vizuri sana ndani Yako mpaka kinakupa nguvu kubwa sana wewe. Ni kutokana na nguvu hii wewe unaweza kufanya vitu vingine vikafanikiwa. Nguvu hii imetokana na mpangilio.

Inalipa sana kuwa na mpangilio na kufanya kazi  Zako kwa namna ambayo ina mwelekeo mzuri.

1. Hatua ya kufanya siku ya leo. Hakikisha kwamba unapangilia ratiba yako ya siku hii ya leo. Pangilia ratiba Yako ya wiki, pangilia ratiba Yako ya mwezi.

2. Usifanye kazi au kitu chochote ambacho hakijapangiliwa kwenye ratiba Yako.

3. Usiruhusu mtu kuingilia ratiba yako ya siku husika

Tukutane kileleni.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X