VITU AMBAVYO WAHITIMU WA CHUO HAWAPENDI KUFANYA INGAWA VINALIPA SANA. 
Habari za siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Imani yangu kwamba siku yako ya leo ni njema sana na unaenda kufanya mambo makubwa sana ndani ya siku ya leo hii.
 
Kila siku ni mpya hakikisha kwmba unaishi kwa namna ya upya na kufanya kazi kwa namna ya upya sana. usiku bali kuwa wa kawaida kwa  kujirahisha hata kidogo. Hata kama mambo yatakuwaje hakikisahw akmmba leo hii unaenda kufanya kazi ambazo umekusudia kufanya na unazifanya kwa bidii kubwa sana.
 
Hakuna mtu ambaye atakuja kwako na kukufanyia kazi ambazo wewe ulipaswa kuwa umefanya. Kama huwezi kuweka juhudi na kuhakikisha kwamba umekuwa vizuri katika kile ambacho unafanya. Kama utaacha hakuna atayekuonea huruma kwamba huajfanya kile kitu. Kumbe hakikisha kwamba unafanya kitu ambacho unapaswa kuwa unafanya kila siku. Kifanye kwa uhakika.
 
Kumekuwa na katabia ambako tayari kameota mizizi yake, ingawa mizizi hii inaweza kung;olewa na kutupiliwa pembeni na kuhakikisha kwamba inejengwa tabia nyingine mpya. Tabia hii imeanza muda mrefu sana na sijajua nani kaanzisha kit kama hiki. Laiti ningekuwa na kutana na mtu huyu, tungeweza kujibizana vizuri. Lakini huyu kwa kuwa mtu huyu siwezi kuonana naye ndio maana nikaamua kuhakikisha kwamba naongea na wewe mwanachuo na wewe ambaye amehitimu chuo kikuu.
 
Kwanza kabisa kwa wale ambao mmehitimu chuo kikuu hongera sana. iwe ni mwaka huu au miaka ya nyuma. Sasa swali langu kwako, je, kwa sasa umeshapata sehemu ya “kujishikiza”? kama bado umesubiri nini? Umemusubiri nani? Kwa nini unajichelewesha?
 
Ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba unatambau kwamba ajira siku hizi zinatolewa ni kidogo sana hivyo wewe unahitaji kuwa mtu wa kufikiri na kuhakikisha kwamba unafanya kwa namna ya tofauti. Hii  ni kauli yangu ambayo siku zote nimekuwa nikiitumia kwa ajiri ya kuhakikisha kwamba unaweza kupiga hatua kubwa sana.
 
Pili kuna kazi ambazo ni habari ya mjini sana siku hizi. Ambazo kama wewe utazifanya zinaweza kukuinua na kukupa mtaji kama mpaka sasa hivi hauna mtaji. Lakini pia zinaweza kukupa pesa ya kujikimu, ukaondokana na hadhi ya kuzunguka na bahasha iliyochoka kwa ajili ya kutafuta kazi.
 
Ndio wewe mkaka, achana kile unakiita kwamba wewe ni mtanashati. Maana sikku zote hakuna utanashati kama hauna pesa.  Kutafuta utanashati bila pesa ni sawa na kusubiria meli airport. Achana  na utanashati shika jembe ukalime. Tanzania ina ardhi kubwa sanakwa ajili yako kuhakisha kwamba unailima na inaweza kukutoa hapo ulipo na kukupeleka sehemu nyingine. Kama mpaka sasa hivi unapoteza muda wako unazunguka na chet, basi ondoka huko, chukua hatua nenda maili za ziada kuhakikisha kwamba umeweeza kupata kitu kingine kizuri sana. anza kwa kulima, shika jembe la mkono na nenda hatu ya ziada.
 
Nyie wadada nani kawaambia kwamba mjini ndio sehemu nzuri kwa ajili yenu kuonesha miguu yenu hiyo. Achana na mambo ya kwamba lazima nikae mjini ili wavulana waone  kisigino changu killivyo cheupe, achana na mambo ya kwamba nataka wavulana waone paja langu. Hakuna mtu ambaye yuko interested na wewe kama hauna pesa. Nenda kijijni ushike jembe na ukalime, maana wahenga walisemakwamba kama unataka mali utaipata shambani. Usitegemee kwamba utajizungusha hapo na watu wakuone mjanja.
 
Hakuna ujanja katika kuzunguka na vyeti. Sio sifa wewe kuhangaika na vyeti vyako, haifai hata kidogo wew kkuzunguka na vyeti wakati unaweza kupika madazzi na ukauza hayo maandazi. Hivyo badili matazamo wako. Maana sikku zote ukibadili mtazamo wako  utakuwa umebadili kitu kikukbwa sana.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X