Habari ya siku hii ya leo Rafiki na ndugu msomaji wa makala za blogu ya SONGA MBELE. Imani yangu leo ndio siku njema sana kwako kwenda kuweka juhudi na kufanya mambo makubwa. Endelea kufanya makubwa mpaka kieleweke.
Kuna watu wamekuwa wakianza kuendeleza vipaji vyao, lakini inafikia hatua vipaji hivyo wanavizima na kuhisi kwamba wamefika. Jambo kama hili limekuwa linawazuia watu wengi kuendeleza vipaji na kuhakikisha wanagusa pale pasipogusika hasa kwenye vipaji vyao.
Kuna watu ambao wamekuwa hawajui ni muda gani wanapaswa kuendeleza vipaji. Ni muda gani vipaji vinapaswa kuendelezwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba inafikia hatua wanaridhika nakuhisi kwamba wana kila kitu.
Lakini leo naenda kukushauri muda sahihi ambao unaweza kuanza kuendeleza kipaji chako.
Muda sahihi wa wewe kuendeleza kipaji chako ni pale unapopatia kitu cha kwanza. Ni pale unapofanya mwendo mzuri na uliokamilika kwa mara ya kwanza.
Kama wewe kwa sasa upo unaendeleza kipaji fulani. Basi usiache kukiendeleza kipaji hicho. Na muda huo ni pale utakapopiga hatua ya kwanza kwa usahihi.
Hapo ndipo utakapotakiwa kuanza kuendeleza kipaji chako.
Kila unapopiga hatua na kuifanikisha, hakikisha kwamba huo unakuwa mwanzo wako wewe kuanza.
Soma zaidi; NIMEZALIWA MSHINDI; Ijue Kanuni Ya Pasi Na Hakikisha Unaitumia
Kazi ya kufanya leo, tafuta jambo dogo la kufanya siku hii ya leo. Baada ya hapo lifanye vizuri. Ukishalipatia, anza tena. Maana mwanzo mzuri wa wewe kuanza ni pale unapopatia kitu cha kwanza kwa ubora hata kama ni kidogo.
Kupata vitabu vyangu BONYEZA HAPA