TATIZO SI RASLIMALI ZILIZOPOTEA-21 Tatizo ni kauli zako


Kila sehemu huwa ina lugha yake ambayo hutumiwa. Nikiwa kidato cha pili mwalimu wangu wa kiswahili alinifundisha kitu kinaitwa rejesta.
Rejesta kwa ufupi ni lugha mahalia.
Ukiwa hospitalini kuna rejesta yake.
Ukiwa sokoni kuna rejesta yake.
Ukiwa shuleni kuna rejesta yake.

Vivyo hivyo katika biashara kuna rejesta muhimu ya kutumiwa.
Rejesta ya biashara ni ya kiupole tofauti na na rejesta ya sehemu nyingine.

Kama wewe huwapokei Wateja wako na kuongea nao vizuri jua kwamba kuna vitu ambavyo utavipoteza.

Unaweza kuwa unajambia kwamba mimi sioni shaka nikimjibu mteja mmoja vibaya si vibaya. Wengine nitawajibu vizuri. Ukimpoteza mteja mmoja jua unaweza kupoteza wateja wote. Kumbuka kuna Wateja wenye uwezo mkubwa sana wa kushawishi watu. Kuna wateja ambao wanaweza kushawishi kundi kubwa la watu na likaacha kuja kwako. Na hao wakiwaaambia wenzao na wenzao wakawambia wenzao yaani utawapoteza wengi. Kuwa makini sana na rejesta ya unayotumia wakati kuongea na watu wanaokuja kwenye Biashara yako. Kumbuka kwamba ni rahisi sana kumpoteza mteja mmoja kuliko ilivyo rahisi sana kumpata mteja mmoja.

kuwa makini kwa upande wa lugha.
Mfano unaweza kumpokea mteja wako kwa lugha nzuri sana. Unaweza kumwuliza nukusaidie nini rafiki yangu. Hakuna mtu ambaye anapenda kuonekana kama mteja. Mteja ni mtu wa muda  baadae anaondoka. Lakini rafiki ni wa kudumu. Waone Wateja wako kama rafiki zako.

Kama hauna bidhaa ambayo mteja wako anahitaji unaweza kumwelekeza kwa lugha safi sana na akakuelewa.
Badala ya kusema, “haloo! hapa umepotea njia, unachokiulizia si mahala pake”
 mwambie “huduma Z kwa sasa haipo, karibu sana siku nyingine itakuwa tayari rafiki yangu”.
Au
“sisi hapa tunatoa huduma ya bidhaa MM, MW, na MK nikusaidie ipi kati ya hizi hapa rafiki yangu”.

Ni kwa jinsi hii utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kumshawishi na kumteka mteja wako.
Kuwa mbunifu kwa lugha unayoitumia. Mara nyingine mteja akifika badala ya kukaa ukiwa umekunja uso kama vile umegombana na mteja wako, unatabasamu. Unaweza kumshika mteja wako kwa kutoa kauli kama hii hapa “karibu sana rafiki, yaani kwa kuangalia sura hii sio ngeni kwangu”. Au kama unamfahamu kwa muda mrefu basi mtaje jina lake halisi. Unaweza pia kumkumbushia juu ya jambo ambalo linamhusu ambalo limetokea siku za hivi karibuni. Jambo ambalo unaona kwa hakika kwamba atalipenda.

Kwa hiyo kiufupi ni kwamba wakati unaendesha biashara yako, jifunze lugha. Jifunze jinsi ya kuwapokea watu.

Jifunze pia jinsi ya kuwaaga wateja wako. Kwa mfano unaweza kumuaga kwa kusema “kwa heri Anita rafiki, bidhaa fulani ikija nitakupigia simu”.

Usipokuwa makini na lugha unayoitumia utawapoteza wateja wengi. Chukulia mfano mteja anakuja kununua Vocha na kukuomba umkwangulie vocha, wewe unamjibu kwa kusema “unadhani waliotengeneza Vocha zisizo za kukwangua walikuwa wajinga, kakwangue mwenyewe”.
Unadhani atarudi mara ngapi kununua kwako?

TUZUNGUMZE BIASHARA

Jipatie nakala ya Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI sasa kwa bei ya shilingi 10,000/-

Lipa pesa kwenda namba 0755848391 jina GODIUS RWEYOGEZA baada ya hapo nitumie email kwa namba hiyo hiyo. Nitakutumia kitabu ndani ya muda kidogo.

Kama umeipenda makala hii jiunge na kundi la HAZINA YETU TANZANIA🇹🇿🇹🇿 upate kujifunza zaidi; http://godiusrweyongeza.blogspot.co.ke/2017/09/hazina-yetu.html?m=1

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
songambele.smb@gmail.com

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X