Ubunifu hupitia katika hatua mbalimbali mpaka kitu kinapokuja kuonekana.
Sio tu suala la kulala na kuamka ukisema mimi ni mbunifu.
Ukizipitia hatua hizi utakuwa mbunifu mzuri sana katika dujinia hii.
1. Hatua ya kwanza ni kutambua.
Hii inaweza kuwa ni
>>>kujitambua wewe mwenyewe.
Wewe ni nani?
Kitu gani ambacho unaweza kukibuni?
Ujuzi gani ulio nao unaweza kukuogezea ubunifu ukawa bora zaidi!
>>>kutambua kile unachohitaji, (je unahitaji kubuni nini?
Mwonekano wake ukoje?
Je,mwonekano unaweza kubadilika baadae?
Kitu gani kinakusukuma wewe kusema hivyo?
2. KUKIFANYIA KAZI. (ACTION)
Ukishatambua wewe ni nani?
Kitu gani unahitaji ili kuwa bora zaidi. Sasa hatua inayofuata ni kufanyia kazi kile kilicho ndani yako. Kuhakikisha kwamba unakiboresha. Hapa utahitaji kutumia nguvu na muda wako kubadili kile kilicho akilini mwako.
Kama akilini mwako kuna mawazo hakikisha kwamba unayafanyia kazi.
Yaweke katika matendo.
3. MATOKEO
Angalia kile kinachofanya kazi na kile ambacho hakifanyi kazi.
kinachofanya kazi endelea nacho.
Kisichofanya kazi achana nacho.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio