Hawa Watu Walipaswa Kuwa Wamefukuzwa Kazi


Kuna watu ambao kwa matendo ambayo wameyafanya waliapaswa kuwa wamefukuzwa kazi na kukosa mshahara wa kampuni ambayo walikuwa wanaifanyia kazi.  Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika dunia hii kuna sehemu ambayo watu wanavumilia makosa hayo na kuna sehemu ambayo watu hawawavumilii makosa hayo.
Moja ya sehemu ambayo watu hawavumilii makosa ni katika ajira. Kama mtu ameajiriwa mwajiri hapendi kuona watu wakikiosea na kufanya kazi vibaya. Kama watafanya kazi vibaya mwisho wa siku watajikuta kwamba wanapoteza kazi zao. Au kwa lugha rahisi ni kwamba watakuwa wamefukuzwa kazini.
Kuna watu ambao mimi naawaangalia leo hii naona kabisaa kama wangekuwa wamejiingiza katika ajira basi wangekuwa wamepotez kazi zao kabisa. Watu ambao wamefanya makosa makubwa sana na dunia ya sasa inawaheshimu wao kama watu maarufu sana. Watu wambao wamefanya makubwa sana.
#1. THOMAS EDISON
Huyu alifanya makosa 10,000. Ndio makosa elfu kumi! Hakuna mwajiri ambaye angeweza kumvumilia mfanyakazi mzembe kama huyu. Yaani umeajiriwa na unafanya makosa 10,000 bila kufukuzwa kazi!!!! Lakini Thomas Edison aliweza kufanya makosa haya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba alikuwa katika ulimwengu ambao unaruhusu makosa. Ulimwengu ambao unachukulia makosa kama sehemu ya kukua. Ulimwengu wa maisha. Tofauti  na shuleni au kazini ambapo mtu ambaye hafanyi kosa ndiye anaonekana ni mtu makini sana.  Katika ulimwengu wa ujasiliamali anayefanya makosa mengi ndiye anakuwa mtu makini sana na kuwa mwekezaji makini sana. Anakuwa mtu mbunifu sana maishani mwake.
#2. CHRISTOPHER COLUMBUS
Huyu naye alifanya kosa kubwa sana. Kama angekuwa ameajiriwa basi angepoteza kazi mara moja. Kosa kubwa alilofanya Christopher Columbus ni  pale alipoenda kutafuta njia ya kwenda india akajikuta yuko katika nchi ya AMERIKA. Hili ni kosa ambalo mwajiri asingweza kulivumilia. Lakini kwa kuwa alikuwa katika ulimwengu wa watu ambao makosa ni sehemu ya maisha basi alijikuta kwamba kosa lake sio kosa. Bali daraja la yeye kuzidi kusonga mbele. Mpaka leo hii anafahamika kwa umaarufu wake wa kugundua ulimwengu ambao hapo awali haukujulikana,
Kumbe tunapaswa kuwa watu wa kuranya vitu mbali mbali na kutafuta vile ambavyo havifanyi kazi. Kama kuna sehemu ambayo haifanyi kazi, basi tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kuirekebisha na kuifanya bora zaidi. Tusikimbie kukosea na kujiona kwamba sisi hatujawahi kufanya makosa wala sisi sio watu wa kufanya makosa.

Badili mtazamo wako ili uweze kuishi maisha yenye furaha kubwa hapa duniani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X