Haya Ndio Matumizi Unayopaswa Kuhakikisha Umeyafanya Kila SikuMara nyingi sana tunafanya matumizi kila siku, kila kunapokucha.  Kwani matumizi ni nini? Matumizi kwa maana ya rahisi ni kiwamba, matumizi ni pesa inayotoka katika mfuko wako. Hivyo kama unafanya mabadilishano yoyote yale ambayo yanahusisha utoaji wa pesa mfukoni mwako jua kwamba unakuwa unafanya matumizi. Mara nyingi sana matumizi haya ambayo yanafanyika ni kwamba huwa yana lengo la kumnufaisha mtu mmoja. Yaani katika kila pesa ambayo inatoka katika mfuko wako jua kwamba kuna mtu ambaye anakuwa ananufaika na matumizi hayo ambayo wewe hapo una kuwa unayafanya.  Kama utanunua nguo kuna ambaye amenufaika na matumizi hayo. Kuna mtu ambaye upande wake wake wa mapato umetuna kwa kiasi kikubwa sana huku kukiwa na mtu ambaye mfuko wake umenyongonyea. Mtu ambaye mfuko wake umetuna ni Yule ambaye unanua bidhaa yeke.

Makala haya hayana lengo la kukutaza wewe kufanya maatumizi isipokuwa ni kwamba yanakutaka wewe uwe makini  katika matumizi ya pesa yako. Kuna mambo mawili ambayo unahitaji kuyafahamu hasa pale linapokuja suala zima la mattumizi ya pesa.
#1. JIFUNZE KUFANYA MATUM IZI AMBAYO YANAKUINGIZIA PESA.
Kuna matumizi ambayo unaweza kuyafanya yakaja na pesa zaidi mfukoni mwako. Kuna matumizi ambayo unaweza kuyafanya na yakakuingizia kipato kwa muda mrefu sana. Haya ni matumizi ya muhimu sana ambayo unahitaji kuyafahamu na ni matumizi ambayo wewe kama wewe hapo unahitaji kuhakikisha kwamba umejifunza na kujua jnsi ambayo yanafanyika.
#2. USINUNUE BILA KUWA NA BAJETI.

Mara nyingi sana watuwengi wanatoka nyumbani wakiwa hawajui wanaenda kununua kitu gani sokoni. Akifika sokoni au dukani akakutana na  nguo nzuri ambayo ameitamani ananunua bila kujua kwamba matumizi hayo hayakuwa sehemu ya bajeti yake ya siku hiyo. Hivyo wewe hapo unahitaji kuwa makini sana na kuhakikisha kwamba kila unapotoka nyumbani unajua kwamba unaenda kununua kitu gani! Ukifika dukani usinunue kwa sababu tu kitu kimeshuka thamani, nunua kwa sababu kile kitu kipo katika  karatasi ya manunuzi ambayo unapaswa kuhakikisha kwamba umeyafanya siku hiyo.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X