Hivi Ndivyo Watu Walio Wengi Wanavyopotea


Kila siku ni siku mpya kwetu sisi kwenda kuweka juhudi na kuhakikisha kwamba tunafanya makubwa. Kila siku ni nzuri na ni siku ambayo wewe unapaswa kuhakikisha unakuwa zaidi ya jana. Kama jana yako ilikuwa bora zaidi ya siku hii ya leo, basi jua kwamba kuna kitu hapa kati kati kati ambacho umepoteza. Au kuna kitu ambacho hujatimiza. Maana siku zote jana huwa sio bora zaidi ya leo.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba leo ndio siku bora sana. Leo ni siku mpya kwetu kuishi hapa duniani. Lakini pia leo ni siku ambayo dunia inaendelea kujizungusha kwenye mhimili wake kwa namna ya utofauti kabisa. Hakikisha kwamba unaitumia vyema siku yako kwa ajili yako, kujiendeleza na kufanya mambo makubwa zaidi.

Turudi katika makala yetu ya leo inayosema kwamba hivi ndivyo ambavyo watu walio wengi wanavyopotea.

Kutokana na ukweli kwamba kila siku huwa inakuja na fursa mpya. Basi kuna watu wamekuwa wakishindwa kuchukua hatua ya kuchagua fursa moja ambayo wataifanyia kazi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hawana mwelekeo maalum. Yaani wanayumbishwa na upepo. Wanaelekea kila sehemu ambayo upepo unawapeperusha ukiwaelekeza.

Hii ndio kusema kwamba ukija upepo wa kusini basi nao huelekea kusini. Ukija upepo wa magharibi basi nao huelekea magharibi.
Lakini kiukweli hali haipaswi kuwa hivi.

Nikiona watu wa aina hii huwa wananikumbusha hadithi ya wanafamilia waliokuwa na safari ya kutembea katika kisiwa kimoja hapa nchini.
Wakati wa safari walikutana na kundi kubwa sana la swala. Dereva wa gari hilo aliawapenda wale swala na kuanza kuwakimbiza. Gari lile halikuwa maalum kwa ajili ya  kukimbiza swala msituni. Alijikuta akikwangua gari. Na mwisho wa siku gari lilianguka kwenye mto mkubwa. Huu mfano unaaksi maisha halisi ya watu walio wengi sana. Yaani  hii ndio kusema kwamba kuna watu wanakimbiza swala kila siku bila kujua.

Sababu kuu inayowafanya watu wakimbize swala ni kutokuwa na Malengo.
 Kumbe lazima uwe na malengo. Lazima uwe na mwelekeo. Lazima ujue unaenda wapi. Na kwa nini unataka kwenda huko. Unataka kwenda na nani.

Kama hautakuwa na Malengo siku hii ya leo utapotea.
Utaishia kukimniza swala badala ya kukimbiza vitu vyenye maana.

Yafanyie hayo kazi mwisho wa siku matokeo makubwa sana yatakuja mbele yako.

Ndimi
Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X