Huyu Ndiye Mtu Ambaye Unapaswa KumwepukaHab ari ya  siku hiii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala haya kutoka katika blogu yako ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako ambapo unaenda kuweka juhudi kubwa sana na kuhakikisha kwamba unafanya makubwa. Siku hii ya leo tusafiri kwa pamoja kwa ajili ya kujifunza kitu kipya chenye manufaa makubwa sana kwetu.
Dunia hii ilianza na watu wawili. Watu wawili wamezidi kuongezeka na kuongezeaka mpaka sasa hivi dunia dunia ina watu zaidi ya bilioni nane. Iliichukua dunia hii miaka mingi sana kufikisha bilioni moja ya kwanza. Baada ya hapo namba ya watu imekuwa ikionngezeka kila kucha. Utafiti unaonesha kwamba kufikia mwaka 2030 basi dunia itakuwa na watu zaidi ya bilioni 10. Hii ndio kusema kwamba idadi ya watu itazidi kuongezeka.

Kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka ndivyo ambavyo na sisi tunazidi kupata watu zaidi wa kuambatana nao. Na mara nyingi wale watu ambao tunaambatana nao wanakuwa na tabia kama za kwetu. Kumbe ndio kusema kwamba linapokuja suala zima la marafiki na watu wa kuambatana nao basi tunapaswa kuwa watu wa kuchagua. Tunapaswa kuchagua kwa sababu marafiki wetu ndio kioo cha tabia zetu. Kama rafiki yako ana tabia mbaya na wewe tutasema una tabia mbaya hata kama utakataa. Lakini ukweli utakuwa unajionesha. Hivyo hakikisha kwamba unakuwa na marafiki ambao kwa hakika watakuwa kioo chako. Yaani hata pale wahenga watakaposema niambie rafiki yako nikwambie tabia yako, hata hutakuwa na hofu kwa maana utakuwa na uhakika kwamba rafiki yako na wewe mnaendana.
Image result for this a person you have to avoid
Leo hii unapoenda kuwaangalia marafiki wako, huku ukiangalia nani ambaye unapaswa kuambatana naye na nani ambaye hupaswi kuambatana naye, hakikisha kwamba haumbatani na mtu huyu hapa mmoja.
Hakikisha kwamba hauambatani na mtu ambaye anakukatisha tamaa.
Kuna mtu ambaye akikusikia tu unaongea kwamba wewe una mpango mkubwa wa kufanya kitu Fulani lazima tu akukatishe tamaa.  Atakwambia kwamba huwezi. Atakwambia kwamba watu Fulani walijaribu na hawakuweza kufanikiwa, atakwambia kamba  tulia kidogo rafiki yangu vitu ambavyo unahangaika navyo hapa duniani ipo siku utaviacha, kwa nini usile bata sasa hivi? Atakwambia leo ni leo asemaye keshoh ni mwongo.

Kama una rafiki  wa aina hii sasa umefika muda wa wewe kuhakikisha kwamba unaachana naye kama unahitaji kutimiza malengo yako mwaka huu. Huwezi kufikia hatua kubwa kimaisha kwa kuendelea kuwa na marafiki wa aina hiii ambao wao wana kurudisha nyuma kila siku. Watu wanajidai wanakuonea huruma kumbea wewe hapo wanakurudisha nyuma. Hivyo nakuomba sana rafiki yangu ya leo hakikisha kwamba haumbatani na rafiki wa aina hii.

Hakikisha kwamba unaweka misingi ya utendaji wako wa kazi. Usiruhusu watu wenye maneno hoasi kuingia katika maisha yako. Kuwa na malengo ambayo unayafuata binafsi na watu sahihi ambao wanaendana na kile ambacho wewe unakifanya utakutana nao njiani. Hiii ndio kusema kwamba wewe hapo ulipo kuna watu maaluma ambao wameandaliwa kwa ajili yako kutimiza malengo yako. Kama utafuata kanuni na taratibu zako bila ya kuzivunja mwisho wa siku watu hawa utakutana nao. kwa leo naishia hapo rafiki yangu. Tukutane kesho kwenye makala mengine kama haya hapa hapa safuni.


Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X