Je, Umesoma Nini Leo?


Habari ya siku hii ya leo Rafiki yangu, imani yangu leo umekuwa na siku njema sana, na unaendelea vizuri sana.

Karibu sana tuendelee kujifunza. Maana hakuna kuhitimu katika kujifunza. Na hapa duniani hakuna aliyehitimu kozi ya kujifunza. Yaani kwamba kahitimu kukutana na watu wapya, kahitimu kuongea, kahitimu kula, kahitimu kufanya kazi kutaja ila machache. Kiufupi watu wa aina hii hawapo hapa duniani. Yaani watu wa aina hii wapo makaburini tu. Kwa hiyo kama wewe unapumua sasa, hauna budi kujifunza kila siku. Yaani kujifunza ni kanuni ya maisha. Kujifunza ni njia pekee itakayokufikisha wewe  unapotaka kufika.

Kama hujasoma kitu leo! Hujaishi leo. Kama hujajifunza kitu leo umejipunguzia miaka ya kuishi.

Soma Zaidi; Vitu Utakavyojifunza Kwenye Kurasa Za Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni

Ukisoma Kitabu kimoja itakuwa kama  umekutana na watu mia moja.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba mwandishi wa kitabu kimoja anakuwa amewasoma waandishi wengi sana kabla ya kuandika kitabu chake.   Hivyo kama utasoma kitabu kimoja cha mwandishi utakuwa na uhakika wa kwamba umekutana na watu wengi sana. Ambao ulikuwa hujakutana na watu.
Je, kuna mbadala wa kusoma? Je, naweza kuacha kusoma  nikaangalia video za you tube na kuendelea na maisha kawaida. Jibu la swali hili ni HAPANA. Tena HAPANA ya herufi kubwa. Soma na kusoma vitabu. Hakuna jinsi ninavyoweza kuiongea kauli hii kwa urahisi ila naendelea kusisitiza kwamba soma, soma, soma. Hakuna kisichowekana. Kama wewe unaona huwezi kusoma kitabu basi naweza kusema umeamua mwenyewe kujizika kaburini  kabla ya wakati. Maana kusoma siku zote kunaweza kukufanya kijana hata kama wewe ni mzee na kutosoma kunaweza kukufanya mzee hata kama wewe ni kijana.

Soma ili upate Maarifa yasiyopatikana kwingine

Soma ili ujitofautishe mwenyewe.

Soma kwa sababu wewe ni kiongozi. Na kiongozi ambaye hajifunzi hafai.

Yaani soma, soma na soma tu!

Soma zaidi; Nijibu sms 1000? Au Nisome Kurasa 1000? Kipi Bora Nifanye Kipi?

Vita


Tukutane siku nyungine kwenye makala ya kuelimisha na kuhanasisha kama haya.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X