Vitu Viwili Vinavyozuia Watu Kuweza Kufikia Malengo Yao


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala haya ya SONGA MBELE. Imni ysngu kwamba umeianza siku yako vyema sana na unaeanda kufanya mambo mkubwa sana siku hii ya leo.
Leo hii tunaenda kuangalia vitu ambavyo vimezuia watu walio wengi kushindwa kufikia malengo yao mwaka huu.
Mwanzoni  mwa kila mwaka watu huwa wanweka malengo makubwa sana ya kufanya mambo makubwa sana, wengi sana huwa wana mpango wa kufanya kitu fulani hata kama huwa sio kwa maandfishi. Wengi sana baada ya siku chache huwa wanapoteza mwelekeao wa malengo yao na hatimaye kuishi ndani ya mwaka mzima bila ya kuwa na malengo. Jambo hili lilmekuwa likifanyika hivi mwaka hadi mwaka. Binafsi nimekuwa nikitaka kujua ni kitu gani ambacho kinawazuia watu walio wengi kuweza kufikia malengo yao kila mwaka. Hapa nimekuja na majibu ya mambo ambayo huwazuia watu walio wengi sana kuweza kufikia malengo. Yasome vizuri na uyafanyie kazi maana kama utaendelea kufanya makosa haya mwaka hadi mwaka hii ndio kusema kwamba itafikia hatua ambapo utyakuwa unalia na kusaga meno kwa sababu tu hukuweza kutimiza malengo yako.

SOMA ZAIDI: Mwanamahesabu Wako Ni Nani?

Image result for why people fail to accomplish their goalsHAWANA PICHA YA WAPI WANAENDA.
Picha moja inaongea maneno mengi kuliko maneno elfu moja. Unapokuwa na picha ya wapi unaenda ni sawa na kusema kwamba hautakuja kukwama njiani kwa sababu zisizo kuwa na msingi, badala yake utazidi kusonga mbela hata pale utakapokutana na vikwazo vya hapa na pale.
Ngoja tu nikupe mfano kidogo wa watu ambao huwa wanakuwa na malengo makubwa sana na hawaachi kwa sababu tu ya kuwa na picha kubwasana kichwani mwao. Watu hao ni wale ambao huwa wanasafiri kutoka eneo moja kwaenda eneo jingine. Yaani huwezi kukuta mtu analalamika kwenye kituo cha basi au bodaboda kwa sababu mvua imenyersa na hawezi kwenda nyumbani kwake. Hii ni kkutokana na ukweali kwambwa anakuwa na picha ya wapi anaenda na matokeao makubwa ambayo atakutana nayo atakapokwenda nyumbani kwake, mtu huyu hawezi kuacha kusafikri na kwenda nyumbani kwake wala hawezi kulalamika kwa kusema  ”unajua mvua imenyesdha na mimi hapa siwezi kwenda nyumabnmi kwangu”. Badala yake atachukua bodaboda na kuhakikisaha kwamba anakwenda nyumbani kwake. Hakuna kisingizio. Hivyo na wewe ukiwa na picha ya wapi unaenda utafurahi sana maisha kwa maana kila wakati autakuwa unajua wapi unaenda na utaaweka juhudi kuhakikisha kwamba umeweza kufikia kule amnbapo unatakiwa kwenda kwa wakati huo,
Jenga picha sasa ya wapi unataka kwenda. Jenga picha ya sasa nani unataka kuwa, jenga pichja sasa ya wewe kama wewe.

SOMA ZAIDI; Mambo Ya Kuzingatia Ili Kuchagua Fursa Sahihi

WANALENGA KIDOGO SANA
Katika maisha unapapaswa kulenga mbali sana hata pale upnaposhindwa kushindwakwako kunakuwa ,mafanikio makubwa sana kwako. Mara nyingi sana watu wanalenga sehemu za karibu sana. Hawataki kulenga mbali sana. Miongoni mwa vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo ni mwonekano wako mkubwa sana wa maisha yako ambao wewe hapo unaouona kwa miaka kadhaa ambayo inakuja mbeleni. hii ndio kusema kwamba mpaka sasa hivi ulikuwa na mpango au malengo ambayo unapanga kuyatimiza ndani yamiaka kumi yarudishe nyuma na pamga kuyatimiza ndani ya mwaka mmoja.
Kama ulikuwa na lengo la kupata shilingi milioni moja mwaka, hakikisha kwamba sasa mpango wako unaukuza mara kumi zaidi. Yaani hakikisaha kwambwa unapanga kupata milioni kumi. Wewe ni zaidi ya ulivyo sasa hivi na unapaswa kufanya makubwa zaidi ya yale ambayo.
Hakikishakwamba unazidisha mipango yako yote mara kumi na zaidi. Hii ndio kusema kwamba haupaswi kulenga na kuweka malengo madoga sana. Wewe una uwezo wa kutimiza malengo makubwa sana zaidi ya yale ambayo umeayaweka kwa sasa hivi.

Nenda kabadili malengo yako sasa na uhakikishe kwamba unayakuza na kuyafanya kuwa malengo makubwa zaidi mwaka huu




Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X